Personal Debts Management Methods

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,459
Reaction score
4,794
Moja kati ya mambo ambayo yanachangia kurudisha uchumi wetu binafsi nyuma ni namna tunavosimamia mapato yetu,matumizi yetu na madeni yetu

Mapato yetu yanaweza kuwa ni faida katika biashara,mishahara na hata dili ndogondogo
Matumizi yetu yanaweza kuwa ya binafsi,ya kifamilia au ya kibiashara
Madeni yetu yaneza kuwa kwa ajili ya matumizi binafsi,ya kifamilia na ya kibiashara

Kwa kuwa elimu ya fedha ni adimu hapa tanzania na hata duniani wengi wetu hatujui namna bora ya kupata na kutumia pesa zetu.Leo nizungumzie jinsi ya kusimamia madeni yako ambalo kimsingi ukilimudu basi unaweza kupiga hatua kimaisha.

Deni ni nini,Deni ni pesa yoyote ambayo unaitumia kabla ya kuizalisha kwa minajili ya kwamba utailipa baada ya kuzalisha kipato.Kimsingi unapoingia kwenye deni unatakiwa utambue tangu mwanzoni kwamba hilo deni litalipwaje.na hapa ndipo umuhimu wa elimu ya fedha unakuja.

Iwapo unakopa kwa ajili ya biashara basi,hakikisa kwamba biashara inao uwezo wa kuzalisha pesa za kutosha kulipa deni hilo na iwapo unakopa kwa ajili ya matumizi yako binafsi basi hakikisha kwamba unacho kipato cha kuweza kulipa deni hilo.

Vile vile unapokopa kwa ajili ya biashar hakikisha unatumia pesa kwenye biashara.Hakikisha unatumia mkopo kwa lengo lililokusudiwa.

Itaendelea
 
Rudi endelee kufafanua, una kimbia nini ? Kuwa mtulivu unapowasilisha jambo muhimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…