Peoples unity for development in africa ni shirika gani?

Omulangi

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
1,036
265
Kuna ofisi zimefunguliwa mikoani mf Kagera Bukoba mjini kwenye majengo ya bohari ya mkoa inaitwa Peoples Unity for Development in Africa. Hawa jamaa wanasema hii ni NGO inakuwa funded na Global network USA. Wanasema inatoa misaada ya kulipia watu karo. Kiwango ni Tsh 570,000 kwa term wale wa primary na 980,000 kwa wale wa sekondari. Sharti ni kuwa mzazi amchangie kila mtoto Tsh 60000 sasa na mtoto ataanza kulipiwa fedha shuleni kuanzia July. Wale wa vyuo na vyuo vikuu watalipiwa Tsh 2,640,000 kwa muhula.
Pia watatoa msaada wa kujenga majumba wa Tsh 6000000 kwa mtu atakayelipia kiingilio cha Tsh 400000. Wenye mashule watapewa Tsh 46,000,000. ikiwa wanalipa kiingilio cha laki sita. Fedha yote wanayotoa si mkopo. Mwanfunzi atakayebahatika kuingizwa katika mpango huu ataendelea kulipiwa kwa miaka 20.
Bronchure yao inasema ofisi zao kuu zipo Tip Top Manzese, Morogoro Rd Usangi House ghorofa ya kwanza. Pia wana matawi Temeke Changombe Rd karibu na shule ya sekoondari Kibasila phone 0787 706802, Ilala Bungoni msaada garage phone 075 222625 , Morogoro ccm house phone 0755 075901.

Watu Bukoba wameanza kumininika kwa wingi kulipa hivyo viingilio ili wasipitwe na bahati hii ya mtende.

Naomba msaada kujua kama hii ni genuine organisation au kuna mtu anajaribu kutafuta karo ya watoto wake? Huko USA kuna hiyo orgnisation inayosaidia katika capacity ilitajwa na hawa jamaa?

Na walio Dar kuna kitu kama hicho?

Omulangi.
 
Ningeomba mwenye kufahamu website au any detail amabayo itatoa mwanga wajambohili. Nimelisikia na lina kamata kasi...!

Is this a genuine thing?
 
Kuna ofisi zimefunguliwa mikoani mf Kagera Bukoba mjini kwenye majengo ya bohari ya mkoa inaitwa Peoples Unity for Development in Africa. Hawa jamaa wanasema hii ni NGO inakuwa funded na Global network USA. Wanasema inatoa misaada ya kulipia watu karo. Kiwango ni Tsh 570,000 kwa term wale wa primary na 980,000 kwa wale wa sekondari. Sharti ni kuwa mzazi amchangie kila mtoto Tsh 60000 sasa na mtoto ataanza kulipiwa fedha shuleni kuanzia July. Wale wa vyuo na vyuo vikuu watalipiwa Tsh 2,640,000 kwa muhula.
Pia watatoa msaada wa kujenga majumba wa Tsh 6000000 kwa mtu atakayelipia kiingilio cha Tsh 400000. Wenye mashule watapewa Tsh 46,000,000. ikiwa wanalipa kiingilio cha laki sita. Fedha yote wanayotoa si mkopo. Mwanfunzi atakayebahatika kuingizwa katika mpango huu ataendelea kulipiwa kwa miaka 20.
Bronchure yao inasema ofisi zao kuu zipo Tip Top Manzese, Morogoro Rd Usangi House ghorofa ya kwanza. Pia wana matawi Temeke Changombe Rd karibu na shule ya sekoondari Kibasila phone 0787 706802, Ilala Bungoni msaada garage phone 075 222625 , Morogoro ccm house phone 0755 075901.

Watu Bukoba wameanza kumininika kwa wingi kulipa hivyo viingilio ili wasipitwe na bahati hii ya mtende.

Naomba msaada kujua kama hii ni genuine organisation au kuna mtu anajaribu kutafuta karo ya watoto wake? Huko USA kuna hiyo orgnisation inayosaidia katika capacity ilitajwa na hawa jamaa?

Na walio Dar kuna kitu kama hicho?

Omulangi.

That is another type of DECI Mzee, hakuna lolote hapo
 
hawa jamaa wapo hapa Dar na wana ofisi zao manzese japo sijawahi kwenda hapo ila nasikia sana matangazo yao redioni hasa redion one asbh,wapo usangi house ukiwa usangi house chini utaona kibao chao.
 
suala linakuja je nao ni mambo ya DECI au?mamlaka husika ni vyema zikafuatilia mara moja,maana tunajua vyombo husika vya serikali tukufu ya mgeni njoo bil mtaji uondoke millionea inasoma hizi hoja sasa hivi tunavyojadili.
 
Kama kweli wanakusaidia kulipia shule ni kwanini uwalipe badala ya kulipa shule moja kwa moja asilimia yako?
 
Ni PUFDIA as an acronym. Msimamizi wake ni Pastor kutoka Uganda. Kwa ufupi mnaliwa ndugu zangu. Yuko jamaa yangu mwaka jana aliwahi kumfahamisha Kamanda Kova juu ya NGO hii. Akaifuatilia akaikuta ina kibali kutoka ofisi ya DCI ya kuchangisha fedha. Vijana wa Kova waliwakamata lakini baadaye wakawaachia. Of course askari wale walilipwa "kitu kidogo". Ukweli huyu akiisha pata fedha za kutosha ni lazmia ataingia mitini. Hizi fedha hazina akaunti anziweka mwenyewe anakojua. Yaani sisi Watanzania ni watu wa kuliwa. Suala la DECI halijakauka tayari kuna hili lingine. Na iweje DCI ndiye atoe kibali cha kuchangisha fedha? Does BOT or CMSA know this? Oh my country Tanzania.
 
Back
Top Bottom