Ndugu yangu miaka kadhaa nyuma ilikuwa kidogo ni- carry course fulani hapo Chuo Kikongwe kwa sababu ya penzi!
Mtoto katoka Arusha, akafikia Mbezi kwa kaka yake, akanicheki jioni kuwa atakuwa free siku inayofuata na bahati mbaya na mimi nilikuwa nina test ya lecturer fulani hivi, mzee mkuda balaa! Nikaona nitatatafuta sababu ya kutofanya test ili nikale good time na Getu wangu.
Mtoto akakubali tukutane lodge, nikapiga hesabu lodge ya karibu nikaamua tukutane mlimani city kisha tukapumzike kwenye lodge zilizopo upande wa pili pale nyuma ya Mlimani city tower(Haikuwepo kipindi hicho)
Nikakutana na G wangu, tukaingia lodge tukafanya yetu; kufika mchana mtoto ananiambia anaomba tulale pamoja usiku huo maana ameaga kuwa atalala kwa rafiki yake na kaka amempa ruhusa. Nikakosa test ya siku hiyo na test ya siku ya pili yake maana nakumbuka tuliamua kukata siku mbili pale.
Niliporudi chuo licha ya Class representative kumjulisha Lecturer kuwa nina udhuru jamaa akakomaa.