MTENDAHAKI
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 4,013
- 1,447
Narejea kauli yako Mh. Rais ya kutofukua makaburi, naandika haya nikiwa nimeuma meno maana hata siyapendi ninayoandika lakini naona ndio njia muafaka! Kichwa huongoza miguu inakotakiwa kwenda!Hakika sasa tunajua tunakokwenda na tunahakika na safari yetu!Pokea pongezi nyingi sana kwa ujasiri wako wa kushughulikia ulinzi wa mali za watanzania. Zaidi ya kuombewa tunatakiwa kukuunga mkono.
Hata hivyo nina ushauri, hawa watajwa (watanzania waliotutia hasara huko nyuma) tukubali walikosea na tuwatake watuombe radhi hadharani, na tuwasamehe!Maana sina hakika kama watatulipa hizo hela (hatujui walipata ngapi?), pia huko nyuma kuna changamoto nyingi ambazo sio rahisi kuzifukua zote na kuzitolea hukumu ya haki leo! Kumbuka anayemlipa mpiga zumari ndio huchagua wimbo! Na kama nilivyoanza kusema kichwa ndio huelekeza miguu iende wapi!
Tuanze upya, tuanzie kwenye marekebisho ya sheria na mikataba kama ambavyo umeelekeza, tuanzie kwenye kujadiliana kulipwa haki yetu toka kwa waliotuibia, na tusonge mbele kizalendo!
Yangu haya kwa leo