PENDEKEZO: Rais Magufuli, anzisha Vijiji vya Ujasiriamali

Jul 14, 2008
1,820
1,032
Wana JF, Salaam sana.

Awali ya wote napenda kutoa pongezi za dhati kwa jitihada zote anazofanya Mh. Rais za kuleta Maendeleo kwa Watanzania.

Imekwisha dhihirika kwa hakika nia yake yeye binafsi ni ya dhati hata kama kunaweza kuwa na mapungufu machache ya kiutendaji.

Ninao uhakika baada ya kipindi cha mpito cha kama mwaka moja au miwili, maendeleo hali za neema itaanza kuonekana wazi kwa kila Mtanzania.

Naongea haya kama Mtanzania nisiye na mlengo wa itikadi yoyote au ubaguzi wowote. Naongea kama mzalendo na nisiyetarajia maslahi yoyote wala fadhila zozote.

Tanzania ni Nchi yenye rasilimali nyingi sana kushinda hata baadhi ya Nchi ambazo kwa miaka mingi zimekuwa Nchi Wahisani kwa Tanzania (Mfano Nchi za Scandinavia).

Utendaji na Usimamizi mbovu pia umekuwa kikwazo kikubwa. Lakini pia ubinafsi na uchu wa kujineemesha kwa kutumia madaraka pamoja na rushwa iliyokithiri ilikuwa pia ni shida kubwa.

Pamoja na yote pia ukosefu wa fikra chanya na kiu ya kutaka maendeleo ikiambatana na uthubutu imekuwa siyo jadi ya Watanzania walio wengi. Watanzania wachache ambao wameweza kuthubutu mafanikio yao yameonekana.

Natumaini kuna baadhi ya Washauri na Wasaidizi wa Rais wanasoma JF.

Pamoja na jitihada za Serikali zinazoendelea, napenda kutoa mawazo yangu machache ni namna gani hatimaye Tanzania inaweza kuwa Nchi yenye Neema kwa kila Mtanzania.

Mpaka sasa Mwajiri Mkubwa wa Watanzania ni Sekta ya Kazi za Asili kwa maana ya Kilimo; Ufugaji; Uvuvi nk. Hata hivyo uzalishaji katika sekta hii siyo wa kiwango cha juu kuweza kuleta maendeleo makubwa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo: Fikra za kutokukuwa na kiu ya maendeleo na kutaka mabadiliko; hamasa za vitendo toka kwa viongozi; mipango madhubuti; mitaji; usimamizi; masoko na mfumo endelevu.

Miaka ya awali baada ya Uhuru; Hayati Mwalimu J.K. Nyerere alikuwa na ndoto za kujenga Tanzania yenye Neema kwa Kuanzisha Vijiji vya Ujamaa. Hata hivyo hili halikufanikiwa kutokana na sababu kadha wa kadha. Baadhi ya sababu hizo ni maandalizi, usimamizi na umiliki wa wazo la Vijiji vya ujamaa kutokukubalika na wanavijiji, kukosa kujenga uwezo endelevu wa vijiji husika nk.

Kwa sasa vijana wengi sana Tanzania wanakimbilia mijini mara baada ya kumaliza elimu ya Msingi na Sekondari na kuacha Wanawake; Watoto na Wazee vijijini na vijana wachache. Hili kwa kiasi kikubwa ni kutokana na ukweli kuwa namna ya kilimo, ufugaji na uvuvi vinachoendeshwa na wengi havilipi. Asilimia kubwa sana ya ardhi ya Tanzania bado haitumiki ukiacha mambo ya mtazamo wa kisiasa. Sidhani kama hata asilima 10% ya ardhi ya Tanzania imetumika.

Napenda kutoa mawazo machache kwa Mh. Rais na Serikali yake:
  1. Vianzishwe vijiji maalumu vya Ujasiliamali (Si vya Ujamaa): katika vijiji hivi uzalishaji ufanyike kwa njia ya kisasa. Mfano: Kilimo cha Umwagiliaji; Bustani; Greenhouses; Ufugaji wa Kisasa wa Samaki katika Mabwawa; Ufugaji wa Nyuki; Ufugaji wa Kisasa wa Kuku; Ng'ombe nk nk.
  2. Serikali ichukue jukumu la kutenga maeneo kwa kuanzia katika kila wilaya ambapo kutakuwa na makazi ya familia zaidi ya 100. Kisha iwekeze katika miundombinu muhimu mfano: Visima virefu vya maji; ili kuhakikisha maji yapo wakati wote.

    Leo hii Saudi Arabia ni wazalishaji wakubwa wa Tende zinazolimwa jangwani huku waki-export tende hizo. Ukweli ni kuwa katika Jangwa wana visima virefu sana vingine zaidi ya kilometre 1 (1000 metres) chini ya ardhi kusaka maji tu. Na kutokana na maji haya wanaweza kuendesha Kilimo. Maji yakipatikana, ufugaji wa samaki, na mifugo mingine pia inawezekana. Hii pia itapelekea kupunguza migogoro ya ardhi isiyo na tija kwani uzalishaji utaongezeka na wengi watajua faida ya kilimo na ufugaji wa kisasa.
  3. Serikali inaweza kama ikiamua kufanya hivyo kujenga nyumba ndogo na za kisasa na za bei nafuu sana kama 100 kila kijiji ambako kila nyumba inaweza kuwa na wanafamilia watano. Na kukawa na vivutio vichache vitakavyowafanya watu wapende kuishi vijijini kama Community Cente ambapo kutakuwa na TV; Viwanja vya Michezo nk. Pia maeneo ya Ujasiliamali kama Wajenzi; maseremala; mafundi mchundo; mafundi baiskeli, pikipiki nk nk.
  4. Serikali ya kijiji itenge maeneo ya kilimo; Ufugaji samaki; Nyuki; Mifugo nk katika kiwango cha biashara. Kwa matumizi ya familia kila kaya inaweza kuwa na bustani na mifugo.
  5. Watu hawa wanaweza kukopeshwa nyumba hizo na wakazilipa katika kipindi cha miaka 10-30 kutokana na uzalishaji katika shughuli zao. Nafahamu hayo ya Serikali kukopesha nyumba yanaendelea katika baadhi ya Nchi kama Rwanda; Namibia nk.
  6. Serikali isiingilie uendeshaji wa kijiji. Ijenge mfumo tu wa Uongozi na Ujasiliamali. kazi kubwa ya Serikali kwa vijiji vya awali iwe ni kutafuta Masoko ya mazao yao na kujenga mfumo thabiti wa kuhakikisha kuwa mazao yote ya kilimo na ufugaji yananunuliwa katika masoko ya ndani na nje. Wanakijiji wawezeshwe pia kuboresha mazoa yao kwa kuyasindika.
  7. Wenye uwezo wapewe nafasi ya kujenga nyumba pia na kuendesha shughuli zao Kijasiliamali. Wanaoweza kujenga nyumba nyingi na kupangisha wapewe fursa hiyo.
  8. Kwa kuanzia Serikali inaweza ikaanza na Pilot Scheme ambapo ikaanzisha vijiji vichache na kuboresha kila mwaka pamoja na kuongeza idadi. Lengo liwe kuwa na vijiji hivi kila kata au zaidi.
  9. Wakazi wa awali wa vijiji hivi waandaliwe kifikra kwa kuhamasishwa na kufundishwa juu ya kufanya shughuli zao kijasiliamali mfano, ufugaji; kilimo nk. Vijiji hivi vitaendelea kukua. Wachahaguliwe kwa kufuata uwiano wa Jinsia na mambo mengine muhimu yatakayozingatia umoja wetu wa Taifa.
  10. TBC1 TV na TBC Radio wawe na vipindi maalumu vya kuhamasisha uzalendo na fikra chanya, ujasiliamali na uzalishaji mara kwa mara badala ya vipindi vingi visivyo na tija.Kunatakiwa mageuzi makubwa sana ya vipindi TBC na wahusika ni vema walione hilo.
  11. Serikali inaweza ikatenga kiasi cha Shs Bilion 300 kila Mwaka kujenga vijiji vya kisasa 30 vya kaya 100 ambayo kila kaya inaweza kuwa na watu 5 (Kila kijiji kukamilika nakisia kiasi cha bilion 10 ila kukamilisha nyumba na miundombinu). Kila Mwaka idadi inaweza kuongezwa.
  12. Wakazi wa awali wapewe malengo ya uzalishaji na wale watakaoshindwa waondolewe. Kuwe na Wataalamu wa kuweza kuwasaidia kufikisha malengo ya Uzalishaji.
  13. Mfumo wa uendeshaji wa Kijiji na maisha uwe wa KIJASILIAMALI.

Haya ni maoni binafsi ambayo yanaweza kuboreshwa zaidi au kujadili changamoto zake.
 
Ni mawazo mazuri lakini pia serikali inaweza kutafuta sector kadhaa kama vile kilimo na kuwa tafuta wafanyabiashara mahiri wa ndani ya nchi na kuwawezesha kimtaji kwa mkopo nafuu ili wawekeze kwa sector husika.

Mfano, kwenye kilimo Bakhresa ama MO wanaweza kuwezeshwa na kufanya kazi hizo.

Kwenye sector ya ujenzi badala ya kutumia Wachina, serikali inaweza kutafuta kampuni hata kumi za ndani na kuziwezesha ili ziwe zinatekeleza kandarasi za ujenzi nk.

Hii itasaidia kuwa na multi-plier effect kwenye sector husika badala ya pesa kwenda nje ya nchi.
 
Mawazo mazuri sana haya.

Mimi ningependa wazo hili hata sasa linaweza kufanya huko huko kwenye jamii kupitia viongozi wa ngazi za chini kama diwani na mwenyekiti wa serikali ya mtaa, badala ya watu kukusanyika kwenye misiba na kutoa fedha kisha fedha hizo kuishia kuliwa na watu hao hao na kuondoka msibani bila kusaidia jambo lolote lile.

Sasa jamii ielimishwe kupigania maendeleo yake.
 
Mkuu, Mtsimbe,

Mawazo yako ndio hata wenzetu kama wayahudi wametumia na hadi sasa kuna maji ya matunda na bidhaa zingine kutoka Israeli kwenye masoko ya Ulaya.

Ulaya na kwingine bado wanahitaji bidhaa hasa za kilimo na ni sisi tu kuhakikisha "branding", "packaging" na "quality" katika bidhaa zetu ndio ufunguo.

Kula tano mkuu.
 
Endapo Watanzania tutakuwa na mawazo kama haya na serikali ikawa sikivu, pale penye kurekebishwa pakarebishwa lazima tufike mbali.

Nia njema ya Dr. Magufuli itaibua watu wengi wenye mawazo mazuri ambao huku nyuma walipuuzwa. Let us hope wanaweza kuyapima maoni haya
 
Tukiweza kufanya yote hayo tena kwa moyo mmoja basi tanzania itahesabika ni nchi moja wapo tajiri duniani. Na sisi tutaanza kutoa misaada hadi nchi za nje.

Nawaza tu lakini nadhani haya mawazo kuja kutimia sio leo. Wala kesho kwasababu.

Mkuu Uko sawa kabisa. Kumbuka mawazo haya tunafanya assumption Kwa maeneo magumu. Lakini kumbuka Tabzania ina maziwa mengi sana Zaidi ya 20 Na mito isiyo Na idadi. Hapa hatujaongelea madini, uvuvi ktk Bahari kuu nk.

Kinachotakiwa Ni Hamasa ya kweli Na mipango madhubuti
 
Mawazo mazuri mnoooo kwa taaifa letu, serikali itasema bajeti haitoshi

Mkuu Kama kutakuwa Na dhamira ya kweli bajeti Ni kidogo sana ukilinganisha Na impact. Watu wanataka kuona mipango ya Maendeleo ambayo itabadili maisha ya watu.

Bado pia ktk hili sekta binafsi inaweza kushirikishwa. Ila mwanzoni kabisa lazima Serikali yenyewe ilisimamie wazo hili
 
Pia waziri wa viwanda na biashara pamoja na wakuu wa mikoa wanaweza kuwa watu wazuri sana kulifanyia kazi hili.
 
Ni mawazo mazuri lakini pia serikali inaweza kutafuta sector kadhaa kama vile kilimo na kuwa tafuta wafanyabiashara mahiri wa ndani ya nchi na kuwawezesha kimtaji kwa mkopo nafuu ili wawekeze kwa sector husika.

Mfano, kwenye kilimo Bakhresa ama MO wanaweza kuwezeshwa na kufanya kazi hizo.

Kwenye sector ya ujenzi badala ya kutumia Wachina, serikali inaweza kutafuta kampuni hata kumi za ndani na kuziwezesha ili ziwe zinatekeleza kandarasi za ujenzi nk.

Hii itasaidia kuwa na multi-plier effect kwenye sector husika badala ya pesa kwenda nje ya nchi.

Mkuu nakubaliana Na wewe. Tukiongeza wigo kuna sekta nyingi sana.

Haiingii akilini nchi Kama Dennark yenye watu wasiopita milioni 10 Na wasio Na rasilimali nyingi kama sisi huku nchi Yao ikiwa sawa Na mikoa yetu michache inazalisha zaidi Na kukusanya kodi kiasi cha kuwa moja Kati ya wafadhili wakubwa duniani Kwa nchi zinazoendelea.

I believe Magufuli administration can bring effective changes. Tuombe tu awe Na team ya ubunifu with positive mind. Baadhi ya wasaudizi wake wanekaa ki copy and paste zaidi Kama waneanshwa toka ktk usingizi nzito. I must be honest Dr Magufuli himself is very honest to whatever is doing.
 
mawazo mazuri sana haya mimi ningependa wazo hili hata sasa linaweza kufanya huko huko kwenye jamii kupitia viongozi wa ngazi za chini kama diwani na mwenyekiti wa serikali ya mtaa , badala ya watu kukusanyika kwenye misiba na kutoa fedha kisha fedha hizo kuishia kuliwa na watu hao hao na kuondoka msibani bila kusaidia jambo lolote lile sasa jamii ielimishwe kupigania maendeleo yake.

Yes Hilo pia linawezekana japo kwa uangalifu sana. Kitu kikubwa Ni maandalizi ya kifikra kabla ya utekelezaji. Then mafunzo ya ujasiliamali Na Kazi Za mikono kutegemea na sekta husika.

Viongozi wengi wa sasa bado wanaongoza Kwa kuzingatia mazoea na mfumo wa zamani. Kinachotakiwa sasa Ni mawazo mapya ya kujenga na usimamizi Mzuri.

Much respect
 
Mkuu, Mtsimbe,

Mawazo yako ndio hata wenzetu kama wayahudi wametumia na hadi sasa kuna maji ya matunda na bidhaa zingine kutoka Israeli kwenye masoko ya Ulaya.

Ulaya na kwingine bado wanahitaji bidhaa hasa za kilimo na ni sisi tu kuhakikisha "branding", "packaging" na "quality" katika bidhaa zetu ndio ufunguo.

Kula tano mkuu.

Richard nakubaliana na wewe.

Kama uzalishaji na usindikaji ukiwa wa juu na Ubora, Africa Nashariki tuna soma la watu milion 150. Last year nilipoenda US for few weeks Uchumi wao uliimorove kiasi kwamba Hata soko la Ndani likawa kubwa. Same to China. TANZANIA tunategemea imports nyingi kuliko exports. Kupitia ubunifu huu hali inaweza ikabadilika. Tanzania could be one of the richest countries in Africa.

Respect Sir!
 
Back
Top Bottom