Napingana na wewe. Hakuna kufungia timu ya taifa maana hakuna kosa lolote walilofanya. Hicho ndio kiwango chao, na ni reflection ya jinsi Watanzania tulivyo.
Badala ya kufungia timu ya Taifa, tuwekeze ktk soka na michezo mingine kwa kufanya yafuatayo kwa uchache kati ya mengi;
1. Tubadilishe sera ya michezo mashuleni ili michezo iwe ni masomo kama masomo mengine (core subjects) sio masomo ya ziada
2. Mashindano ya shule za msingi sekondari na vyuo iwe ni lazima kufanyika kila mwaka na walimu wa michezo mashuleni wawe na taaluma
sio volunteers
3. Timu zote za ligi kuu ziwe na timu za vijana na bajeti ya kuendeshea timu za vijana zipitiwe na kuhakikishwa na TFF
4. Timu za vijana ziwe na ligi, sio bonanza la wiki 2.TFF itafute hata utaratibu wa timu kuchezwa kwa gharama nafuu kwa mfano kwa kanda
5. Iwe ni marufuku ligi kuu na ligi daraja la kwanza kuchezwa kwenye viwanja visivyo na nyasi nzuri na vyoo. Ukiacha viwanja vya Dar es Salaam na Zanzibar, viwanja vya mikoani vyenye hadhi angalau kidogo kuchezewa ligi kuu ni Sokoine, Kambarage, Mwadui na CCM Kirumba. Navyo viongezwe thamani hasa nyasi za kuchezea
6. Tushiriki mashindano yote ya vijana kwa ngazi zote na kwa uaminifu mkubwa bila kujaza vijeba. Mashindano kama Challenge Cup tutumie zaidi timu za U-20, U-23 na wazoefu
7. Tuendelee kujenga weledi ktk uendeshaji wa mambo yetu, hatua kwa hatua, geuza klabu ziwe makampuni, ongeza kiwango che waamuzi, n.k
UKIFANYA HAYA NDANI YA MIAKA 10 HALAFU TUSIWE NA MAENDELEO YA MAANA BASI TUTAKUWA NA SABABU YA KUACHA KABISA MASUALA YA SOKA
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.