PCCCB CHUNGUZENI RUSHWA KITUO CHA POLISI NZOVWE- MBEYA

amshapopo

JF-Expert Member
Sep 7, 2014
1,651
3,815
Hiki kimekua sio kituo tena bali ni duka. RUSHWA IMEZIDI. Mtuhumiwa anakamatwa rushwa inatolewa anatoka. Mshitakiwa akienda kushtaki rushwa lazima ikutoke.

kwenye kituo hiki cha nzovwe kuna kichochoro pembeni ukipita huitaj kuuliza. Magari, boda boda zinavyokamatwa maeneo ambayo kunavituo yanaletwa nzovwe. Tusaidieni PCCCB tumechoka kwani tokea kituo kimefunguliwa 2007 mkuu wa kituo ni huyo huyo.
 
duh hayo ma C mbona mengi mdau?? au taasisi imebadilisha jina
 
Hiki kimekua sio kituo tena bali ni duka. RUSHWA IMEZIDI. Mtuhumiwa anakamatwa rushwa inatolewa anatoka. Mshitakiwa akienda kushtaki rushwa lazima ikutoke.

kwenye kituo hiki cha nzovwe kuna kichochoro pembeni ukipita huitaj kuuliza. Magari, boda boda zinavyokamatwa maeneo ambayo kunavituo yanaletwa nzovwe. Tusaidieni PCCCB tumechoka kwani tokea kituo kimefunguliwa 2007 mkuu wa kituo ni huyo huyo.

Watakua wamesikia, maana wengi wamo humu.
 
Kuna tatizo kubwa zaidi ya maelezo kwenye wizara ya mambo ya ndani, hasa jeshi la polisi kuliko maelezo mtu awaye yote awezavyo kutoa. Huo ni mchezo wao, hiyo ndiyo inayowaweka mjini. Bahati mbaya sana watumbua majipu ni wanufaika wakubwa na mfumo polisi uliopo unaoitwa policcm. hawa jamaa ni wapigaji wa kawaida tu. mkiwakuta barabarani mtadhani watu, kumbe siyo kabisa!
Sijui nani atatuokoa na janga hili la policcm! Sioni jitihada zozote za kurekebisha mambo kwenye jeshi hili lisilowajibika kwa maslahi ya umma.
 
katika mazingaobwe ambayo serikali haiwezi fanya ni kwa taasisi ya rushwa kuwakamata polisi kwa rushwa. mambo yao huwa wanamalizana wenyewe kwa wenyewe...mkilalamika sana pccb wanamwita ocd na kumpa majina ya askari wanaotuhumiwa kwa rushwa halafu ocd ana malizana na askari wake
 
Waacheni polisi wanasaidia wananchi, pccb wadili na wakwepa kodi wakubwa na wala rushwa
 
RPC Ahmed Msangi atumbue jipu aibu mkoani kwako! Salaam zikufikie hapo ulipo watakuharibia kazi!!!
 
Back
Top Bottom