Juzi nilifungua pc yangu pia sababu feni ilikuwa inapiga kelele na pc inashika moto mpaka kuzima yenyewe pia ilikuwa na vumbi hivyo nikaiweka sawa na kutoa vumbi ila baada ya kuifunga kila kitu kila nikibonyeza powerbutton laptop inawaka bila screen alafu inazima hapohapo ndani ya sekunde na feni inazunguka na kuzima pia.
Nimejaribu ile option ya kuizima na kutoa battery kisha unashukilia power button kwa dk 1 lakini hali iko vilevile.
Nimejaribu kutoa cmos battery na kuirudisha baada ya saa 1 moja labda ingereset bios settings lakini bado inafanya vilevile.
Ila baada ya kuona hivyo ikabidi niangalie ile fluid kwenye proccesor na graphics card nikaona yote imekauka kabisa sababu hapo kabla ilikuwa inashika moto mpaka inazima yenyewe.
Je hilo linaweza kuwa tatizo?
Hapo wakati nasafisha feni nilikuwa natumia chaji kuiwasha then narekebisha feni mpaka ilipokaa sawa na ilikuwa inawaka vizuri na nilikuwa makini kutosababisha ESD.
Kuhusu ram na hdd nahisi ni vizima sababu vyote niliviondoa mpaka battery kabla sijafungua.
Pia mwanzo ilikuwa ukiondoa ram zile led lights za keyboard na power button vinawaka kasoro screen pekee ila sasa hivi hata ukiweka ram au usipoweka zile led lights zinawaka na kuzima hapohapo.
Ukiweka chaji inaonesha kama chaji inaingia bila tatizo.
Laptop haitoi beep yoyote ile.
Ila kama motherboard imeungua si ni kwamba pc inakuwa haiwaki kabisa hakuna led lights wala sign za chaji yaani imekufa kabisa au inakuwaje mkuu?
Kama motheeboard ndio tatizo je kuliplace na kununua mpya au used inaweza kuwa bei gani?
Hapo nini tatizo mkuu?
Laptop ni hp Elitebook 840 g2.
Chief-Mkwawa msaada wako mkuu.