Kama ilivyoada katika kuelimishana masuala ya pc gaming leo naomba nitoe somo kidogo kuhusiana na PPSSPP FOR WINDOWS 1.4.2
Kwanza tujue hii ppsspp ni nini
PPSSPP hii ni emulator y psp, ambayo kazi yake kuu ni kuemulate psp games ziweze kucheza katika pc windows and mac.
Kwa kutumia ppsspp unaweza cheza game yoyote ile ya psp katika pc yako.
Unachotakiwa kufanya ni, kudownload ppsspp for windows iliokatika format ya zip au exe then utainstall katika pc yako na kuenjoy psp games katika pc yako.
Kwa kutumia ppsspp unaweza cheza addictive games kama God of war chain of olympus na God of war ghost of sparta, Need for speed carbon, Need for speed Most wanted na nyenginezo nyingi.
Vilevile ppsspp inakupa uwezo wa wewe kutumia usb pad controllers kucheza ambayo inasaidia kuziua uharibifu kwa keypad katika pc yako
Karibuni katika ulimwengu wa pc gaming na ppsspp
Sent using
Jamii Forums mobile app