Eraldius
JF-Expert Member
- Jun 17, 2011
- 1,122
- 911
Paza sauti okoa watu wako
MAWAZO YANGU LEO TAR:14/01/2017
Nimekuwa nanyi katika jukwaa hili kwa kipindi sasa tukishirikiana katika mijadala mbali mbali lakini haya yote yakiendelea nimeona nivema kupitia ninyi niwashirikishe nilichowaza na nilichojifunza katika miangaiko ya maisha ndani ya wiki mbili. Kwakweli hali ya maisha ya wananchi wa kawaida sinzuri kiuchumi kuanzia uzalishaji mali mpaka umilikiji mali namengine mengi. Hii ni hali ambayo nimekuwa nikiishuhudia hapa Mwanza katika baadhi ya maeneo ila ikaja kunipa msukumo wa kuona haja ya kuandika Makala hii baada ya *Tarehe 5 January 2017* kusafiri kuelekea mkoani Kagera hali ambayo nimeikuta kule inasikitisha. Nikaona hili linaweza kuwa ndani ya uwezo wetu kila mmoja bila kujali shughuli, muda, imani , itikadi yake kisiasa N.K. Katika maeneo tulipo turipoti taarifa za hali ya maisha ya maeneo husika. Hii itasaidia Serikali kupata pakuanzia ( *penye matatizo makubwa* ) katika kuwasaidia watu wake au kuwaelekeza kipi chakufanya.
Kumewahi kuwepo na harakati nyingi za namna hii kwenda kwa Serikali na Idara zake na wengine wakaenda bali kwa kuanzisha *Hashtag* mbali mbali katika mitandao mbalimbali ya kijamii tukipaza sauti na tukaona matokeo *chanya*. Sasa itoshe tuone kuna haja yakwenda upande mwingine wa kamera kwa namna ile ile.
Ikumbukwe Tanzania nikubwa na *Mh. Rais JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI* hawezi kuona au kusikia kero za maeneo yote na kama anaweza kuzipata au kuzisikia kupitia wawakilishi wake zinaweza kuwa naupotoshaji ndani yake. Tufanye haya tukielewa dhamira yake katika kuliletea taifa letu maendeleo hivyo itasaidia kumshirikisha kuona maendeleo ya watu na vitu katika Taifa Letu. Pia tusifanye haya kwa mwenendo wa kujitafutia umaarufu kisiasa au Kijamii bali tusukumwe na utashi wa Utaifa na Uzalendo.
N:B Tunaweza kuripoti kwa kuandika au kurekodi *SAUTI/VIDEO* za mahojiano na wananchi wenyewe na kama kuonesha kero za Vitu mf. barabara tutumie *picha na video*.
Shughuli hii pia iende sambamba nakufichua Uhalifu katika maeneo yetu pia kuonesha kazi nzuri au mabaya za watendaji wake katika Halimshauri / Wilaya, Mikoa, Majimbo N.K . Hii itakuwa chachu ya uwajibikaji na Raia kufata sheria na kuliletea Taifa letu maendeleo.
TANZANIA MPYA NA YA VIWANDA ITAJENGWA NA SISI WENYEWE KWA KUSHIRIKIANA
Mawazo yenu yanahitajika katika hili
Nawasilisha