GE2025 Paul Mwakajumba atoa wito kwa madiwani wateule kujipanga kuleta kura za kishindo kwa CCM nchi nzima

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,428
Ndugu Paul Douglas Mwakajumba, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa 2022 - 2027 kutoka Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya ametoa pongezi kwa Madiwani wa Kata zote nchini kwa kuteuliwa kugombea nafasi za Udiwani huku akiwasihi kuwa wasiishie tu kufurahia kuteuliwa kugombea bali kwa sasa wajikite zaidi kuweka mikakati ya kukiletea ushindi Chama Cha Mapinduzi (CCM)

"Pamoja na salamu napenda kutumia nafasi hii adhimu kuwapongeza wateule wote kwa nafasi ya Udiwani Nchi nzima ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hasa katika Wilaya yetu pendwa na Jimbo letu la uchaguzi la Kyela lililopo Mkoa wa Mbeya"

"Ndugu zangu, ma Cde wa Chama Cha Mapindunzi (CCM), huu siyo muda wa kushangilia kwa kuteuliwa na kuaminiwa na Chama kupeperusha bendera ya Chama kwa nafasi ya Udiwani, ni Muda wa kutafakari kazi kubwa na majukumu mazito yaliyo mbele yako, kwanza kutafuta kura za kishindo kwa Chama Cha Mapinduzi kwa ngazi zote, Kwa Rais, Mbunge na wewe Diwani"

"Pili ni muda wa kuandaa mpango kazi wako wa namna utakavyoenda kuwatumikia wananchi kwa kuzingatia ahadi zako wakati wa kampeni na ILANI ya CCM 2025 - 2030.
Tukumbuke Kwa pamoja tutashinda, umoja wetu ndiyo ushindi wetu kwa Chama Cha Mapinduzi."

"Naomba makundi yote yazikwe maana hivi sasa tunakipigania Chama Cha Mapinduzi ili tupate ushindi wa kishindo kwa CCM. Tayari tuna Mteule wetu kwa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, ambaye ni Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na mgombea mwenza ni Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, kule Zanzibar tunaye Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ila kwa nafasi ya Ubunge bado tunasubilia nani atateuliwa ila kwa Udiwani ni wewe Diwani Mteule"

"Hongera sana na ninakupongeza Hivyo basi wakati ukifika wa kampeni , twendeni kwa wananchi kama CCM na siyo MTU maana hakuna aliye juu ya Chama Cha Mapinduzi na Mungu wa mbinguni awabariki sana, Ahsanteni!"

Kazi na Utu, Tunasonga Mbele!
Kidumu Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Cde. Paul Douglas Mwakajumba
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa 2022 - 2027.

 
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…