Paul Makonda: Hata ningepata sifuri kwenye masomo yangu, bado ningekuwa Mkuu wa Mkoa

Kishimbe wa Kishimbe

JF-Expert Member
Jul 18, 2013
4,662
4,162
MAKONDAA.jpg

KUHUSU ELIMU YAKE
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amefunguka tuhuma zinazozushwa kupitia mitandao ya kijamii na watu mbalimbali kuhusu elimu yake na zinazoeleza kuwa amefoji cheti cha mtu mwingine.

Akizungumza kwenye kikao cha kamati ya ushauri wa Mkoa (RCC) RC Makonda ameeleza kuwa kinachogombaniwa siyo Makonda bali ni kiti alichokalia (UKUU WA MKOA), hivyo ameeleza kuwa nafasi yake ya ukuu wa Mkoa amepewa na Mungu.

Pia amfafanua kuwa hata kama angepata sifuri au daraja la kwanza katika masomo yake, Mungu angetaka awe Mkuu wa Mkoa angekuwa tu, kwani Mungu ndiye anapanga kila kitu na kuongeza kuwa yupo imara kuliko alivyokuwa jana.

KUTISHWA KWA WAZAZI WAKE
Pia RC Makonda amefunguka kuhusu kutishwa kwa baba yake mzazi, pia kuna watu walikwenda eneo analoishi baba yake na mama yake mzazi na kupiga picha, ili wakaoneshe nyumba anayoishi mzazi wake.

KUHUSU KUITWA SHOGA NA MGUMBA
RC Makonda ameeleza kuwa watu wamekuwa wakimtolea lugha chafu kuhusu uzazi wake na kumuita mgumba kwa kuwa hana mtoto na wengine wamekuwa wakimuita shoga, amefunguka na kusema kuwa haoni tusi jipya.

RC Makonda amesema ipo siku watu wataulizwa kuhusu matendo wanayoyafanya duniani kilasiku, hawana budi kuwa makini na matendo yao.

KUHUSU DAWA ZA KULEVYA
RC Makonda ameeleza kuwa tangu aianze vita ya dawa za kulevya yameibuka mengi na kusisitiza kuwa hatoacha ataendelea kwani wapo wanaoshukuru kuanza kwa vita hiyo na kuhoji kwanini haikuanza mapema kwani imeokoa maisha ya wengi, kuhusu maendeleo ya vita hiyo RC Makonda amesema kuwa mashamba ya bangi yanateketezwa kila uchwao, siku mbili zilizopita wamekamatwa watu 100 na kete 400 za dawa hizo pia zimekamatwa.

Chanzo: Swahili news
 


Ndugu zake na Daudi Bashite wameona isiwe tabu, Ngoja wamsaidie kumjibia Daudi Bashite wao baada ya jamaa kuchomekwa msumari kwenye kidonda kibichi.

wakaandaa habari uchwara na kutupia kwenye Blog.

Nashauri Bashite arudi shule kuristiti...njia pekee ya kujibu mapigo ya Mchungaji wa Yesu!
 
Mi nilitegemea aje na kanusho na kusema vyeti vyangu halali ni hivi hapa na sikuwahi kupata zero na jina langu halali ni hili hapa.

Unakuja na very cheap argument eti nafasi ulipewa na Mungu.. So Stupid..!!
Yaah Mungu siku zote ndio hugawa riziki.. But be a man.. Respond to your allegations!!

Daudi Albert Bashite jibu tuhuma kwa KUKUBALI au KUKATAA na sio kumchanganya Mungu kwenye Uhalifu wako wa Taaluma..
 
Vyovyote iwavyo. Mh RC Paulo aachane nao provided elimu yake iko straight forward kwenye taratibu za Utumishi wa Umma. Na ushauri wangu awakate kilimilimi kwa kuweka wazi qualifications zake na naamini he can do that to silence the movie. Go go RC
 
Back
Top Bottom