Gorgeousmimi
JF-Expert Member
- Jun 21, 2010
- 9,296
- 7,713
Tupe kimoja kimoja 🙂Subira ni ibada.
nafikiria kisa,maana vimejaa kwenye tenga
Sawa nakusubiri ustaadh Mkoroshokigoli!!Kuwa na subira gorgeousmimi
Hellow wapendwa wangu,
Leo ningependa tuongelee kuhusu subira.Kama wahenga wetu walivyosema subira huvuta kheri.
Wanaadamu tulivyoumbwa ni viumbe wenye parapara na tuko katika matabaka tofauti.Kuna wale watu ambao wakitaka lao ndo wamelitaka na kuna wale walojaaliwa subira na uvumilivu.
Wapendwa wangu tunapaswa kuwa na subira kwani changamoto zote tunazopitia katika heka heka zetu za kila siku ni kipimo cha imani yetu.Usipoteze imani yako na uvumilivu kwani ni vitu hivyo ndio vitakavyokupa nguvu ya kusonga mbele."EVERYTHING HAPPENS FOR A REASON"
Tuepuke kuhukumu kwa dhana tu bali tuwe na subira na kuamini kuna malengo ya kila kitu katika maisha yetu .Dhana ni kitu ambacho hata dini imepinga hilo.
Ningependa leoleo tufunguke kuhusu mikasa tofauti ilotukuta katika maisha yetu ambayo ikapima imani zetu pamoja na subira zetu.Tujifunze kupitia kwako.
Karibuni sana
Wasalaam gorgeousmimi
Nice post ........
Nitarudi....
Umenifanya nikumbuke maneno ya mwandishi Ngugi Wathiong' aliwahi kusema" despair is unforgiven sin"
Pia nimeyakumbuka maneno ya mwanamama wa kisenegali katika kitabu chake cha "Such along letter"(Barua Ndefu kama hii) aliwahi kusema
"wakati una maamuzi yake, wakati una kanuni zake, mpaka kanuni zake zitimie ndio wakati utende ila sisi binaadamu tunapenda kuulazimisha wakati utende sasa... "
Subra ni kipimo cha namna gani binaadamu yupo madhubuti katika kuyaendea mambo yanayomkabili.
Sawa nakusubiri ustaadh Mkoroshokigoli!!
gorgeousmimi ujumbe mzuri sana wa kuwajenga kisaikolojia wale waliokata tamaa na kupoteza tumaini baada ya kuondokewa na yale yaliyokuwa na thamani kubwa sana ndani ya mioyo yao......
Pole sana Be strong!!Nyc post, though bado niko kwenye maumivu yakiisha nitakuja kushare.