Wakati Acacia ikifungasha virago, tukumbushane mambo ya kijinga tuliyokuwa tunafanya mgodini

Huku mlikuwa mnafanya kazi kama peponi, Taa, Lift, Mashine nk

Mererani kule kushuka tu chini ni machimbo baadhi yana Monorok (Winchi) zinazo tumiwa kupandisha vifusi duniani

Hakuna cha taa wala mavazi maalumu, ni wewe na tochi yako na kujipanga mstari kusomoa viroba, Compressor ikizima wakati Nobel ashaseti mambo yake hewa ya sumu lazima iwaue, mvua ikinyesha maji yanawashukia, Vifusi kufunika watu ni jambo la kawaida
Msosi wenyewe sasa upige ugali maharage saa tisa mchana kumi na mbili mzame kutoka kesho yake saa tano asubuhi
Ushirikina wa ajabu unaweza kuwa umepumzika kusubiria hewa chafu ivutwe duniani basi milio ya chatu ukiwasha tochi huoni kitu

Dah wachimbaji wadogo wana tabu sana na kwa hakika tunahitaji wawekezaji wakubwa ili kufanya uchimbaji wenye tija

Kaburu wa Tanzanite one yeye alikuwa ana enjoy tu uchimbaji wa kisasa ila ndio hivyo katauchia mashimo na hela yake nchi haijafaidi

Inauma sana
 
bora huko kwenye dhahabu
mi nikikumbuka tanzanite 1 huwa naogopa na kufurahi kwa wakati mmoja!sitausahau mgodi wa main shaft hasa siku skip ukute haifanyi kazi unatakiwa upande kwa miguu!mgodini kuna raha yake bana ila ngema zikishuka ndo huwa mtafutano

Master nilikua natafuta information za kuingia mgodi wa tanzanite yani kama inawezekana mtu kufanya visit na kujifunza vitu mbalimbali vya mgodini
 
Huku mlikuwa mnafanya kazi kama peponi, Taa, Lift, Mashine nk

Mererani kule kushuka tu chini ni machimbo baadhi yana Monorok (Winchi) zinazo tumiwa kupandisha vifusi duniani

Hakuna cha taa wala mavazi maalumu, ni wewe na tochi yako na kujipanga mstari kusomoa viroba, Compressor ikizima wakati Nobel ashaseti mambo yake hewa ya sumu lazima iwaue, mvua ikinyesha maji yanawashukia, Vifusi kufunika watu ni jambo la kawaida
Msosi wenyewe sasa upige ugali maharage saa tisa mchana kumi na mbili mzame kutoka kesho yake saa tano asubuhi
Ushirikina wa ajabu unaweza kuwa umepumzika kusubiria hewa chafu ivutwe duniani basi milio ya chatu ukiwasha tochi huoni kitu

Dah wachimbaji wadogo wana tabu sana na kwa hakika tunahitaji wawekezaji wakubwa ili kufanya uchimbaji wenye tija

Kaburu wa Tanzanite one yeye alikuwa ana enjoy tu uchimbaji wa kisasa ila ndio hivyo katauchia mashimo na hela yake nchi haijafaidi

Inauma sana

Duuh ni noma sana mkuu...nataka informations za kutembelea migodi ya Tanzanite mkuu
 
Part I nilielezea namna tulivyokuwa tunajituma na siku nyingine tunaamua kutofanya kazi (kuzuga) ili kupumzisha miili yetu kutokana na kazi nzito na hatari za ku operate Jackleg machine, kupanda ngazi 18 zenye futi 12 kila moja huku mgogoni umebeba vifaa mbalimbali kama vile ANFO (Unga wa kulipulia/blasting materials, detonators na vifaa vya kujiokolea ambavyo hutakiwi kuvivua muda wako wote wa kazi....

Niliahidi kuwaletea ni WAPI WAFANYAKAZI HUJISAIDIA, WAPI UTAKIMBILIA ENDAPO ITATOKEA HALI YA HATARI KAMA VILE MOTO, KUFUNIKWA KWA NJIA YA KUTOKA MGODINI KUTOKANA NA KUPOROMOKA KWA MWAMBA AU TETEMEKO LA ARDHI, TARATIBU ZINAZOFUATWA ILI MGODI ULIPULIWE KWA SHIFT HUSIKA NA MAMBO MENGINE KIBAO likiwemo kwa nini mikataba ya wafanyakazi wa underground Bulyanhulu huwa haina mwisho (maoni yangu) Inaendelea..
9a00fb069edfffa06a934a5b92a4f19a.jpg
22952ecb3747db2e8310ef42b01ce859.jpg
f3867fa1a96cf7f0c677ea8175b9f733.jpg


HHUDUMA YA KUJISAIDIA

Pamoja na wingi wa wafanyakazi, chakula kizuri kilichokuwa kinatolewa na kampuni ya SODEXHO na baadae AKO Cantering company limited mgodini hapakuwa na sehemu maalumu ya kujisaidia!! Ilikuwa tukibanwa haja tulikuwa tunaenda vilipo vifusi (makinikia ) tunajisaidia hapo au kwenye Mill hoe (Mill hoe) ni Shimo ambalo linachimbwa kutokea level moja juu hadi level nyingine kwa ajili ya kuporomosha blasted material ili yaje yachotwe na mashine kubwa kama Scoop na kutolewa nje kwa mtambo unaokimbia kwa kasi kubwa hadi process plant.

AJALI ZINAZOTOKEA MARA KWA MARA MGODINI

Hadi naacha kazi mgodini ni wafanyakazi wanne walipoteza maisha on the spot nikiwa niko Bulyanhulu. Ajali nyingi mgodini zinatokea kwa sababu za kuangukiwa mwamba, kugongwa na mashine, kubanwa na mashine, kukatika kwa mtarimbo wakati wa ku drill na kulipukiwa na milipuko kimakosa.

Ajali ambayo sitaisahau ni ile ya rafiki yangu........... na wezake wawili kwa wakati mmoja na wakiwa pamoja . Hawa walifunikwa na kifusi kirefu ambacho kilifunika eneo lote walipo, njia zote za kuwaokoa zilishindikana hadi ikaitwa rescue team toka South Africa hata walipofika tayari ndugu zetu hawa walikuwa wamekufa na kuharibika vibaya.

Baada ya mwezi mmoja niliandika barua ya kuacha kazi na ukiandika barua ya kuacha inakupasa ufanye kazi mwezi mmoja mwingine kutokana na mkataba ulivyo.

SEHEMU ZA KUJIOKOA KIPINDI CHA HATARI
Unapokuwa Chini underground unakuwa na mtungi wa hewa wa kukusaidia endapo itatokea sitofahamu. Huu unakuwa umejifunga kiunoni na upo mahususi kwa ajili ya kukufikisha kwenye CHUMBA CHA KUJIOKOA KILICHOPO HUKO CHINI (Refugee Chamber)

Hivyo unatakiwa kujifunga pua ukipumua kwa kutumia huo mtungi na kukimbilia chumba hicho salama ambacho kina kila vifaa kikiwemo chakula special ambacho hata ikibidi wiki nzima uko huko ukisubiri kupata usaidizi.

Vyumba hivyo vipo kila level ya mgodi (kila sehemu ya ghorofa ya mgodi) lakini kutokana na tabia mbaya za ma miner vyakula vinavyowekwa humo huwa vyote wamefungua na kula!!!

JE, USHAWAHI KUJIULIZA KWA NINI DHAHABU HUHUSISHWA NA IMANI ZA KISHIRIKINA? JE UNACHUKUA MUDA GANI HADI URUHUSIWE KUFANYA KAZI CHINI YA ARDHI TENA ZAIDI YA KILOMETA MBILI CHINI!? JE KWA MLIOFANYA KAZI.

BULYANHULU HASA CONVETIONAL DEPARTMENT MNAIKUMBUKA ILE SEHEMU AMBAYO UKIKAA HAPO LAZIMA UNIGWE BILA KUMUONA ANAYEKUNIGA? MIE NILINIGWA Uamini au usiamini.

Itaendelea part III.

MODS kama inafaa unganisha na part I.

[HASHTAG]#Moscow[/HASHTAG] mn [HASHTAG]#jogi[/HASHTAG] [HASHTAG]#kelvin[/HASHTAG] marcus [HASHTAG]#option[/HASHTAG] [HASHTAG]#castr[/HASHTAG] [HASHTAG]#kilambimkwidu[/HASHTAG] [HASHTAG]#hibiscus[/HASHTAG] interior [HASHTAG]#mwamba028[/HASHTAG] [HASHTAG]#kibumbu[/HASHTAG] [HASHTAG]#ISO[/HASHTAG] M. CodD
 
Aisee nimeipenda hebu uiendeleze mkuu. Japo nimemshikia zamu mkuu flani kwa leo atanisamehee mr Jv.

Subscribed

Part 2 plzzz

Mnajisaidia wap huko ndan?

Hyo pati tuu lini mkuu ngwapanagi

Unga humu usisahau kunitag

Duh aiseeee hii tamu saaaana sitamani kuikosa, Ng'wanapagi usisahau kuintag mkuu

Dah! Mkuu nami unitag

Nadhani Part II ianzishie uzi wake.
Nimeshatupia part II
 
stori nzuri nimependa

lini mkuu

Hapo kwenye mambo ya Ushirikina hapo asilimia 90% wanashiriki..
Mambo ya NDAGU noma sana

Huu uzi uendele tafadhali

Mleta uzi uko underground nn

Nimechukua kiti kabisa mkuu kujua kifuatacho

Sasa mkuu siuendelee kusimulia

Nasubir part two


Mleta mada kakimbia
Nishatupia part II
 
Back
Top Bottom