Parking fees Dar, zimekuwa kero kwetu wenye magari

Atlantis Voyager

JF-Expert Member
Jan 19, 2018
367
500
Kila eneo ambalo ni la kupaki magari na imefika mpaka nje ya nyumba zetu utaona kijana amevaa reflected coat na kimashine.

Wenzetu Afrika hii hii unalipa parking imejengwa kwa lami na surveillamce camera zipo. Kitendo cha ku declare parking at yout own risk wakati unachajiwa ni wizi na dhuluma.

Natoa mfano mwenge maeneo ya nakiete au mwenge Bakery ya waturuki kwenye chuo cha boston. Mnachaji parking wakati hata paving hamkuchangia hata senti moja ni dhuluma
 
Mkuu acha gari nyumbani panda mwendokasi mbona mwake tu Gari tumia kwenye mizunguko yako ya kawaida au siku ukiwa unatoka na familia.
 
Mwendokasi ilishaondoka na JK. Sasa hivi imekuwa kero kama mabasi ya kijiji.

Tiketi feki, vyoo sijawahi kuona abiria wanatumia. Yanajaza kupita maelezo wakati afrika hii hii mabasi ya abiria yana grade. Luxury coach inakuwa nauli bei juu na haisubiri ijae.

Huu mradi umetushinda watu weusi
 
mimi kwenye hili nahisi wamiliki wa magari tunatakiwa kuwa wakali lasivyo tutaonewa mpka basi.kwa mfano mimi huwa silipi kabisa tozo za kipumbavu kama hizi za kwenye maeneo ya biashara hasa baa au migahawa ya chakula.kuna wengine hukaa kwenye parking za majengo yenye huduma za kijamii na ni parking za jengo husika mfano pale mawasiliano tower.wanatakaje hasa,kwamba ukitaka huduma sehemu hizo usiende na gari au ukifika pale ukunje gari lako uingie nalo ndani?
 
Halafu hizi hela hatujui zinaenda wapi. Na hii Chui security ya Kina seven mosha naona ndio kinara wa kuchaji parking fee hatujui kama hela kweli zinafika maana hata kununua paving au kuweka lami hatuoni.

Chui security wame kamata parking zote za shopperz, Mlimani na maeneo ya wazi.

Nadhani serikali ijenge parking maalum kama za airport ndio wachaji na sio mitaani.
 
Mkuu acha gari nyumbani panda mwendokasi mbona mwake tu Gari tumia kwenye mizunguko yako ya kawaida au siku ukiwa unatoka na familia.
Acheni majibu ya reja reja, mleta mada ana hoja ya msingi kabisa kama huna positive thoughts kula kimya wengine watiririke.
 
Mkuu jibu gani sasa hapo la reja reja ushauri mzuri pia kama ataufatilia utampunguzia pia ata cost licha ya kumpunguzia usumbufu anaoupata.
 
Halafu hizi hela hatujui zinaenda wapi. Na hii Chui security ya Kina seven mosha naona ndio kinara wa kuchaji parking fee hatujui kama hela kweli zinafika maana hata kununua paving au kuweka lami hatuoni.

Chui security wame kamata parking zote za shopperz, Mlimani na maeneo ya wazi.

Nadhani serikali ijenge parking maalum kama za airport ndio wachaji na sio mitaani.
Halafu Hazina security eti parking fee wakati risk zote ni za kwako.Kweli GARI ni Ngombe,mjini ukikoswa na wazee wa brush,wa parking lzm wale
 
Back
Top Bottom