Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha Cecilia Paresso amewaomba wananchi wa jimbo la Kakonko kumchagua Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kile alichoeleza kuwa mgombea huyo ana sifa zote za kuiongoza nchi.
Paresso ameyasema hayo Oktoba 12 alipokuwa akizungumza na wananchi wa jimbo la Kakonko, mkoani Kigoma.
"Dkt Samia Suluhu Hassan ana uwezo na sifa za kutosha na kutuongoza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" amesema Paresso