Panya mjanja

Panya mjanja

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,539
Reaction score
4,854
PANYA MJANJA.





1)Tulidhani wewe mwema,kumbe kiburi mdudu.
Siyo mtu ni mnyama,uliekufa kibudu.
Timua mkata pema,hakuna wa kukumudu.
Ondoka panya mjanja,ewe joka mataifa.



2)dunia wauma uma,wewe ni sumu mdudu.mzee mtakia mema,siyo wa zama za jidu.
Ewe farao jipima,uwatesa mahudu
Ondoka panya mjanja,ewe nyoka mataifa.



3)aso kujua ni nani,labda nduguyo shetani.
Muingilia shimoni,chunguza watu ya ndani.
Nge asie shimoni,mtotoye yu njiani.
Ondoka panga mjanja,ewe nyoka mataifa.



Shairi=PANYA MJANJA.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160.
iddyallyninga@gmail.com
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom