Panya alimeza kipande cha dhahabu
mwenye dhahabu akachanganyikiwa
na kuamua kumkodi mpelelezi mmoja
ili aje amuue panya aliyemeza
dhahabu. Mpelelezi alipofika alikuta
panya zaidi ya 500 lakini alishangaa
kumuona panya mmoja
kajitenga,ndipo alipomkamata na
kumuua,alipompasua akakuta kipande
cha dhahabu akamkabidhi
mwenyewe.Yule jamaa alipigwa na
butwaaa huyu mpelelezi alimjuaje yule
panya ikabidi amuulize.
Jamaa:aisee we mkali,ulijuaje kama
huyu ndiye panya aliyemeza dhahabu?
Mpelelezi:hawa panya nao ni kama raia
Watanzania wakiwa na mali hujitenga
na wenzao.