Mtetezi.com
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 3,134
- 3,579
Habari za muda huu wanajamvi!
Ninaamini kuwa wengi wetu tunaelewa mambo mtambuka yanayoendelea ktk nchi yetu, leo tuanze na hili nalo ni issue ya kupiga vita madawa ya kulevya sisi watanzania tumekataa kabisa kutoa ushirikiano hata wa kimawazo tu na tumeamua kusimamia matakwa na mslahi yetu huku wengi wetu tuna watoto na wadogo zetu ambao huenda wana au wakatumbukia ktk ulevi huo!
Mimi kama mchambuzi na mwanaharakati mwanzoni wakati picha linaanza nilishangazwa na approach aliyoitumia mkuu wetu wa mkoa kutaja vidagaa laa hasha wote hapa thread zilijaa zikisema mh aache kutaja vidagaa ataje mapapa na ndivyo ilivyosemwa hata na wabunge wetu!
Baada ya awamu ya kwanza kuisha mh akaja na baadhi ya mapapa hiyo haikuwa na mstuko sana bali awamu ya nne imeleta mvurugano na mpasuko mkubwa kati yetu kwani tumeamua kuwatetea watumiaji na wauzaji kwani ni vipenzi wetu, maboss wetu na viongozi wetu!
Napata tabu sana kuamini kuwa eti watanzania tumeamua kusema kuliko wapenzi wetu, maboss wetu na viongozi wetu waguswe bora swala hili life!
Wanafalsafa wengi walishawahi kunukuliwa wakisema yakuwa eti siasa ya mtu mweusi ni siasa chafu ila kiasili ya siasa sivyo ilivyo.
Nihitimishe kwa kusema kuwa sisi kama watanzania wazalendo tunapaswa kushirikiana na yeyote yule atakayejitolea kupigania mustakabali wa tanzania kwani kwetu sisi tanzania ni kwanza dini, vyama,wapenzi,team zetu zitakuja baadae.
Ww kama mtanzania chukua muda kutafakari hatma ya tanzania ya ww na wajao achana na ushabiki kwani wengi wetu tumekuwa tunashabikia tu na mwishowe tunaumia.