Pale siasa safi na uongozi bora kinapokuwa ni mtihani

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,072
Serikali yetu ya awamu ya 5 imekuwa naa changamoto sana ktk nadharia hizi mbili za siasa safi na uongozi bora!
Ccm ya awamu hii imekwama ktk siasa!
Ushahidi:-
  1. Matatizo ya uchaguzi kwa Zanzibar na hili la Dar es Salaam
  2. Siasa za kuchafuana hata wenyewe kwa wenyewe. Kama utawakumbuka walivyoanza kutumbuana na kuwaadhibu watumishi wa umma! Leo mwanasiasa akiondoka ktk nafasi yake akili inayokuja kuwaa ametumbuliwwaa! Ana makosa ktk utendaji kitu ambacho kinawatesa wachache waliotumikia taifa lao kwa awamu zilizopita!
Uongozi bora nao hamna kwa kiasi kikubwa!
Kiongozi ni team maker!
Kiongozi anasaidia waliopo chini yake na ndiye muongoza dira!
Nini linatokea awamu hii:-
  1. Viongozi wamekuwa kama viranja wa zamu! Wao ni kushtukiza kufukuzana! Tutumie case 3, waziri Mkuu anaambiwa mtu kala rushwa, haoji na wala hatoi nafasi ya utetezi anafukuza! Kigwangala eti kwa kuwa wauguzi hawakumtaja mwenzao fukuza wote na makonda kwa kuwa nimefika ktk kikao kabla yenu basi ocd weka ndani hawa!
  2. Mrejesho wa kasoro za kikazi haufuati taratibu za kikazi! Mfano. Waziri anashutumiwa kwa rushwa anakurupuka na kujitetea kwa media hasa Twitter na Instagram! Waziri anafukuza watu, lkn wanaporudi maeleza anayatolea Twitter!
  3. Kuna mapungufu ya watendaji na vitendea kazi. Viongozi wa leo badala ya kuwasaidia watumishi kwa kutoa lugha zenye kuboresha na kuwasaidia wananchi waelewe, wao wanatoa lugha chochezi kati ya RAIA na watumishi! Mfano. Kila mtu anajua uhaba wa dawa hospitalini, au uhaba wa walimu na vitendea kazi, badala ya waziri mwenye dhamana ku-take responsibility yeye anakandamiza kwa mtumishi. Mwl Nyerere alilazimika kuwaambia wananchi wafunge mikanda! Hapa aliwasaidia watumishi kwa kuutangazia umma kuwa hali si njema lkn si awamu hii! Kila tunapokwama ni sababu ya watumishi Ila serikali ipo perfect!
My take: siasa safi na uongozi bora ndiyo misingi mikuu ya maendeleo! Wanasiasa mnategemea sana ufanishi wa taasisi nyingine na watumishi wa umma!
Siasa za unafiki, uongo na kuwagawa wananchi hazina tija!
Ila bahati mbaya, uongozi si "KAZI TU" ni busara na uwezo wa kubalance uhalisia na mahitaji halisi ya mwanadamu!
Mahitaji yanaweza kuwa = walimu wanatakiwa wapate nafuu ya usafiri hivyo wapande mabasi bure
Uhalisia = serikali haina mabasi yake yenyewe na hivyo serikali labda iombe wananchi wajitolee, walimu watambue hii changamoto au mabasi yaondolewe baadhi ya kodi kufidia gharama za uendeshaji! Vinginevyo walimu wafunge mikanda!
Tutende haki kwa kila upande! Natural justice iwepo hata kwa dhalimu yapaswa kusikilizwa kwanza!
Hata Mungu mwenye uwezo alisikiliza utetezi wa Adam kabla hajamtoa bustani ya Eden! Mungu aliuliza Adam uko wapi? Mbona umejificha? Lengo ni kumpa chance Adam ajieleze na si kwamba tunaweza kujificha mbele ya Mungu wetu!

Hebu viongozi mjitahidi kupunguza mihemko na mtende yaliyo mema!

Haya na mengine mengi yanaweza kufanyiwa kazi endapo tutazingatia utawala bora na siasa safi!
 
Siasa safi na uongozi bora vimefeli kote CCM na Chadema ....walau mpaka sasa JPM anafukia mashimo kidogo ....
 
Siasa safi na uongozi bora vimefeli kote CCM na Chadema ....walau mpaka sasa JPM anafukia mashimo kidogo ....
Ni kweli, Ila uongozi wa ccm kwa kuwa ni chama dola una impact ya moja kwa moja na wananchi! Ukawa wao impact yao ni indirect!
 
Siasa safi na uongozi bora vimefeli kote CCM na Chadema ....walau mpaka sasa JPM anafukia mashimo kidogo ....
Mtazamo, that's too low for you....

Mtoa mada ametoa hoja with concrete examples and constructive ideas ni vipi twaweza fikia mafanikio...

Wewe umerukia kwenye mambo ya chadema na CCM wakati hoja ni mwenendo wa serikali... Unaonesha una chuki iliyopitiliza kwa hao chadema kiasi cha kuwa kipofu...
 
msalimie fisadi lowasa we nyumbu
Rahisi sana kuona kuwa kila anayekosoa Jambo ni mtumishi wa Lowasa!
Lazima ujifunze kuona maisha beyond ccm!
Lazima ujue ultimate goal ktk siasa kwa mwananchi si chama X kushika dola, Bali ni kuwa na mafanikio ktk maisha yake! Kuleta maendeleo ktk jamii yake!
Pole kama bado unaishi maisha ya kampeni hadi leo!
 
lowasa aliwafanyanga nini nyie?
Achana nae huyu mkuu, ukiangalia muda aliojiunga JF na mashambulizi anayotoa kwa Lowasa na chadema utagundua ni wale wanaosubiri ajira#46 anataka yeye apate cheo kikubwa kuliko wenzake. Ni wa kumpuuza tu huyu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom