Padri feki anaswa Morogoro!

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,685
Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Joseph Hat Asenga, aliyefika Parokia ya Mt. Maria Madeko ya Morogoro na kujitambulisha kuwa yeye ni Padri na ametokea Marekani amekuwa akifanya kazi zake nchini Marekani, Jimbo la New York.

Padri huyo feki amekamatwa,baada ya jeshi la Polisi kushirikiana na uongozi wa Parokia ya Mtakatifu Maria Modeko iliyopo Kata ya Mazimbu Morogoro, akiwa na Majoho Saba ya Upadri.

Akiwa na vifaa mbalimbali, pamoja na vitambulisho feki, Padri huyo feki alikamatwa March 5, SAA 10:30 jioni.

===============
===============


Jeshi la Polisi mkoani Morogoro, linamshikilia mkazi wa Manispaa hiyo, Josephat Asenga (47), mwenye taaluma ya uhasibu, kwa tuhuma za kujifanya Padri.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo, alisema kuwa, Asenga alikamatwa juzi saa 10:30 jioni, katika maeneo ya Modeco, Kata ya Mazimbu katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Maria.

Kwa mujibu wa Kamanda Paulo, mtuhumiwa huyo alifika parokiani hapo Juni mwaka jana akiwa amevaa mavazi ya Padri na kujitambulisha kwa Paroko wa parokia hiyo, Malt Dyfrig Joseph, kuwa yeye ni Padri anaishi Jimbo la New York Marekani.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, baada ya kujitambulisha kwa Paroko huyo na kuonesha kitambulisho chake, alimuomba Paroko huyo kumpangia zamu ya kuendesha Misa ya Jumapili iliyofuata na kukubaliwa na Paroko huyo bila kukagua vizuri kitambulisho chake.

Alisema mara baada ya misa hiyo, Paroko alipata taarifa kutoka kwa msamaria mmoja wa Kituo cha Amani cha Chamwino mjini hapa, kuwa Padri huyo feki anaishi na mwanamke katika maeneo ya Ujenzi kinyume na taratibu za upadri.

Baada ya kupata taarifa hizo, inadaiwa Paroko huyo aliwaomba waumini wamshawishi Padri huyo feki, afike parokiani hapo na baada ya kufika, alihojiwa na Paroko huyo na kudai kuwa alipata upadrisho katika Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, baada ya Paroko huyo kupata maelezo hayo alifanya mawasiliano na Katibu wa Jimbo hilo la Dar es Salaam na kujibiwa kuwa hakuna jina la Padri huyo.

Juzi Alhamisi majira ya saa 10:30, Padri huyo feki alimpigia simu Paroko huyo na kumuomba ampange kuendesha Misa Takatifu ya Jumapili parokiani hapo, na kukubaliwa na paroko huyo na kumtaka afike kanisani.

Baada ya kufika, taratibu za kujulisha Polisi zilifanywa na askari walipofika kanisani hapo, walimkamata mtuhumiwa huyo.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo, baada ya kufanya mahojiano na mtuhumiwa, alikiri kuwa yeye sio Padri na walipokwenda nyumbani kwake kwa ajili ya kufanya upekuzi, walimkuta akiwa na majoho saba ya upadri.

Mtuhumiwa huyo ameendelea kushikiliwa Polisi na atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika

Chanzo: MtizamoHuru



 
Hii ni hatari sana.
Walimshitukiaje?
 
Huyo Padri feki alikuwa hajui taratibu za Kanisa katoliki! Anafikiri wakatoliki wanakurupuka kupokea wageni ovyo, sasa ameumbuka!!
 
Ukiwa Padre wa kweli utatambulika mahali popote hata bila kuwa na majoho.
 
Mojawapo Ya Kanuni Ya Padri Wa Kikatoriki Ni Kuwa Na Sala Kila Siku Saa Kumi Na Moja Alfajiri Kabla Ya Kwenda Kuadhimisha Misa.KIFUPI WANALATIBA YAO AMBAYO HUFANANA.
 
Angalia USALAMA WA NCHI, ACHA MADHARA KWA MASISTER YASINGOTOKEA WANA MAADILI MEMA WALE NDO MAANA YA NADHIRI ZAO
 
Kuna mzazi mmoja feki anaitwa baba wanne wakati baba O.G wa wanawe wanajulikana, ngoja niwauzie issue polisi!
 
Huyu padri feki angetakiwa kupiwa kichapo kwanza kabla ya kukamatwa .
 
Mojawapo Ya Kanuni Ya Padri Wa Kikatoriki Ni Kuwa Na Sala Kila Siku Saa Kumi Na Moja Alfajiri Kabla Ya Kwenda Kuadhimisha Misa.KIFUPI WANALATIBA YAO AMBAYO HUFANANA.

Ina maana walimu wa somo la kiswahili hawapo tena mashuleni au inakuwaje? Kwenye R unaweka L na kwenye L unaweka R
 
padre dizaini hii ndo hua wanawagegeda masista
 
Nasikia ni zaidi ya mara mbili kasalisha na pia ameishafungusha ndoa moja sasa sijui ni ukweli au tetesi za waumini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…