Ashura9
JF-Expert Member
- Oct 21, 2012
- 740
- 485
Our President JPM is a Wonderful President! Yaangalie haya pia
Yaani kitendo cha kuwapigia Clouds 360 simu na kuwapongeza sio cha kawaida kwa Rais kukifanya lakini Raisi wetu mpendwa JPM amekifanya na nilikuwa shocked! yaani sikuamini maskio yangu lakini ni kweli kabisa tukamsikiliza vizuri na akampa simu mkewe Janet the First Lady, hapo tukajua kweli ni Raisi aliyekuwa akiongea; Hii inadhihirisha kuwa Raisi anatusikiliza wanyonge kupitia vyombo mbalimbali, na hivyo ni budi basi tujitahidi kuandika mambo ya msingi yanayohitaji kutumbuliwa mbali na yale ya maisha ya kawaida.
Pongezi sana kwa Raisi kwa hilo, endelea na uzi huo huo wa kutumbua ila tukumbuke wananchi wako kwa kutatua matatizo yanayotuhusu kwa karibu kama

- matatizo ya ardhi,
- urasmishaji wa ardhi ambao ulianza na haukuisha maeneo mbalimbali ya Dar
- Umeme bei kuupangda kila leo na kukatikakatika
- Udhibiti wa mishahara ya kampuni za binafsi gap kubwa kati ya wananchi na wageni
- Kodi kubwa ya PAYE
- Jipu la NHIF: kutoza kiwango kikubwa sana cha kujiungwa kwa watu binafsi ambao pia ni watanzania na pia kuwatenga: kama huna 1,000,000 huwezi kujiunga, sasa mtanzania wa kawaida hapa mjini atapata wapi hiyo hela?, watanzania ndio walipa kodi sasa kwa nini NHIF ijali zaidi wafanyakazi wa serikali wanaotumia kodi zetu na isiwajali watu wengine wa mijini?
- kodi ndogondogo za wafanyabiashara wadogo ziondolewe au kupunguzwa
- Mfumo wa kupata leseni ya biashara ni tete
- Matatizo ya upatikanaji wa maji
- Udhibiti wa bei mbalimbali za vyakula - watu wanajiuzi bei za ajabu hata kama bei zimeshuka kama vile sukari bado sh 2,300/-
- Udhibiti wa nauli za mabasi na daladala bado ni tata
- Udhibiti wa uzoaji taka uwajibikaji wa serikali katika hili
- udhibiti wa dawa mahospitalini na maduka ya dawa ya binafsi bado ni jipu mfano nilikuwa hosp ya kisarawe haina dawa ya aina yoyoye ilibidi kununua dawa kwa duka la pembeni mwa hospital, na hospitali nzima haina mashine ya kupima sukari ilibidi kumpigia simu daktari anaetembea nayo mfukoni na hakupatikana, mgonjwa wako anasubiri dr ambae hajulikani yuko wapi, vipimo mwisho saa tano asubuhi sasa kama mgonjwa wako kazidiwa saa sita itakuwaje??. na pia wodi zimecraki wakati ni mpya na wodi iliyotakiwa kujengwa ya ngorofa moja imejengwa vyumba vitatu vya wagonjwa na hii ndio hospitali ya wilaya ya kisarawe!
- Bei za hospitali za private zidhibitiwe pia
- Pensheni za wazee haziongezwi inflation bado wanalipwa hela ileile kama miaka kumi iliyopita
- Ajira nafasi za kazi kutolewa kwa kujuana no transparency
- nafasi za kwenda kusoma kwa scholarship za nje za serikali ziwe wazi pia hutolewa kwa kujuana; zitangazwe kwenye vyombo vya habari kwa kila mtu kusikia
- Uzimwaji wa simu ni jipu, watu tayari wanamizigo ya simu madukani, wananchi wamesha nunua haileti tija kusema mwisho mwezi wa sita. Iwe baada ya kugundua simu feki mwezi wa sita watu wapewe muda kujipanga hiyo ndio fair