Sasa hivi mabanda katika eneo la Temeke hospitali kuna usafishaji ya hali juu sana huku vibanda vyote vinaondolewa kando kando ya barabara katika mitaa yote.
Hii ya 'kuongeza wahalifu mtaani' imekuwa wimbo wa kisiasa, na wabongo mkikaririshwa kitu hakitoki kichwani, hata kama hakina msingi. Vibanda vyote viondolewe, magereji bubu yote yatolewe, mitaa inyooke jiji lipate hadhi. Watu wajifunze kufungua biashara katika maeneo rasmi, watambulike na walipe kodi kama watumishi wa umma wanavyolipa kwa lazima. Bila kutumia nguvu wabongo hawana aibu, watakupangia mafungu ya vitunguu hadi airport!