ze kokuyo
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 7,417
- 9,603
Operation Mole Cricket ni kampeni iliyofanywa na Israel dhidi ya Syria kuharibu Mizinga ya kutungulia ndege iliyo karibu na mpaka wa Israel pia ndani ya Syria.Hii ni operation ya kwanza ya kijeshi katika historia ambayo ilihusisha jeshi la anga lenye vifaa na teknolojia ya magharibi kuharibu kabisa mizinga yenye makombora ya kudungulia ndege yaliyotengenezwa na Umoja wa Kisovieti(USSR).
Pia ni moja ya mapambano makubwa kabisa ya anga tangu vita ya pili ya Dunia na makubwa tangu yale ya vita vya Korea. Jeshi la anga la Israel lilianza kubuni na kutengeneza teknolojia na vifaa vya kuharibu mizinga ya kudungulia ndege tangu mwisho wa vita vya Yom Kippur.Mwaka 1980,joto la mvutano kati ya Israel na Syria juu ya Lebanon lilivyozidi kupamba kupanda iliwafanya Syria kuweka mizinga yenye Makombora ya kudungulia ndege katika eneo la Beqaa Valley. Juni 1982, Jeshi la Israel likavamia Lebanon huku mivutano yake na Syria ikiendelea, hii ilifanya Israel kuanzisha oparesheni ya kuharibu sehemu zenye Mizinga ya kudungulia ndege(Suppression of Enemy Air Defences{SEAD}).
Asubuhi ya Juni 9 1982,ndege za Israel ziliruka huku zikigawanya nyingine zikiruka karibu na usawa na ardhi, nyingine kati(10000m) na juu kabisa ambapo ilikuepo ndege maalumu kabisa ya kusaidia kuziongoza ndege zinazoenda kushambulia iliyojulikana kama Hawkeyes. Ndege hizo ziliruka kimakundi ikijumuisha F15 na F16 ambazo zilikua 96 ikijumuisha kundi la kwanza na kundi lingine likijumuisha ndege za mashambulizi ya ardhini a in a ya F4 phantoms ambazo zilikua 92.
Ndege hizo za Israel zilikua zimefungwa mitambo maalumu ya kieletroniki ambayo kazi yake ni kuzidanganya rada za adui au kuzizima kabisa zisiweze ona kitu.Upande wa Syria ulijumuisha ndege aina ya Mig-21,Mig-23 na Sukhoi 20 zaidi ya 100.Ndege za Syria zilitegemea data/taarifa kutoka kwenye vituo vya ardhini huku zile za Israel zikitegemea E2C Hawkeye.Mizinga ya kutungulia ndege ilijumuisha ile ya SA-2,SA-3 na SA-6.
Mapambano yalianza baada ya Israel kutanguliza ndege isiyo na rubani(drone) kuelekea Syria ili iweze kuonyesha mahali ilipo mizingaa ya kutungulia ndege baada ya kushambuliwa huku F15 na F16 zikilinda ndege za mashambulizi ya ardhini aina ya F4 phantom dhidi ya mashambuliz ya anga kutoka kwa ndege za Syria.Baada ya Syria kuitungua ndege isiyo na ruban ya Israel, ndege za Israel zilianza kushambulia mizinga ya kutungulia ndege kwa makombora aina ya UGM-78 na makombora maalumu ya kuharibu mizinga ya kutungulia ndege aina ya UGM-45.
Upande wa Syria kwa majibu walirusha makombora 56 kutoka mizinga ya kutungulia ndege lakini haikufanikiwa kulipua ndege hata moja ya israel.Baada ya mashambulizi kuzid kua mazito upande wa Syria waliamua na wao kurusha ndege zao aina ya Mig-21,Mig-23 na Sukhoi 20 kujibu mashambulizi ya anga ya Israel.Baada ya muda mfupi ndege za Syria zilianza kushambuliwa na zile za Israel F15 na F16 kupitia taarifa kutoka kwenye ndege yao aina ya E2C-Hawkeye ambayo ilikua ni maalumu kwa ajili ya kuziongoza ndege za Israel wapi pa kushambulia na wapi adui alipo.
Mpaka kufika jioni jumla ya mizinga 17 kati ya 19 ya kutungulia ndege ya Syria ilikua imeharibiwa kabisa na ndege 29 aina ya Mig zilikua zimeharibiwa kabisa na ndege za Israel.Mpaka kufikia usiku jeshi la Israel lilikua limeharibu kabisa kituo cha mawasiliano cha jeshi la Syria pamoja na mizinga mingine minne yakutungulia ndege.
Mpaka asubuhi ya siku inayofuata jeshi la Israel lilikua limeharibu mizinga 30 ya makombora ya kutungulia ndege ya jeshi la Syria pamoja na ndege zaidi ya 100 za jeshi la syria nyingi zikiwa zile za mashambulizi ya angani aina ya Mig-21 na Mig-23 huku upande wa Israel ukiwa umepoteza ndege moja isiyo na rubani pamoja na ndege mbili aina ya F15 zilizokua zimeharibiwa kidogo.
Baada ya mashambulizi hayo Marekani iliamua kuweka maridhiano ya kusitisha mapigano kwa pande mbili Israel na Syria.
MWISHO.

Attachments
-
images-5.jpg8.3 KB · Views: 227
-
images-2.jpg8.1 KB · Views: 220
-
images.jpg7.5 KB · Views: 212
-
download-1.jpg5.3 KB · Views: 199
-
images-4.jpg4.6 KB · Views: 197
-
images-1.jpg7.7 KB · Views: 286
-
download.jpg4.6 KB · Views: 198
-
300px-USN_E-2C_Scewtops.jpg9.9 KB · Views: 214
-
download-2.jpg4.8 KB · Views: 242