bongo hiyo bwana mkubwa!😀😀Wajameni!!!
Nimehamia sehemu moja hapa wilaya ya kinondoni ni pazuri sana!!! Kinachonisikitisha ni namna ambavyo mbele ya nyumba yangu kuna open space lakini kuna jamaa (wala haishi hapa) amefungua karakana ya cerpentry na watu wa welding, pia ameweka mgahawa na vitu kadha wa kadha
Hakuna choo wala vyoo, muziki ni mpaka basi lakini kila ninapofuatilia serikalini, tena hasa baana ya mkuu wa wilaya kuahidi kuondoa biashara sehemu zisizo rasmi, naambiwa tena na wakuu wa pale kwamba waondoke waende wapi? subiri uchaguzi nk.
Ombi langu kwenu ni ushauri wa kitalaam hasa kwennye rights zangu, financial implication kama naruhusiwa kushitaki au kudai fidia, haki ya wale wanaofanya biashara na uingizaji wa siasa kwenye mambo yaliyo serious
Nimeileta huku kwani naona it had to be dealth professionally kuliko kisiasa
I need you help
wakuu wa wilaya wenyewe hawa makada waliofeli maisha na genge la wanajeshi wastaafu, sioni muwajibikaji zaidi ya walaji na genge la mafisadi.Cha msingi ni kuendelea kuwabana hao jamaa wa Halmashauri, kwani Mkuu wa Wilaya atabase zaidi kisiasa. Zaidi jaribu kuangalia ramani ya eneo hilo ili kuweza kujenga hoja ya nguvu ya kubadilishwa kwa matumizi ya eneo.
Huu utaratibu wa kuvamia open spaces uliasisiwa na CCM! Sehemu nyingi zilizokuwa zimetengwa kama open spaces zilivamiwa na CCM na kuanza kufanywa vitega uchumi vya hao mafisadi kama vile maegesho, kumbi za starehe, maduka, bar n.k.
Utamaduni wa bustani Nhi hii haupo! Angalia pale Mnazi mmoja ni kinyaa tupu!
Tunakaribia Miaka 50 ya uhuru lakini ni porojo tu zinazotawala! Tumeshindwa hata kupanda maua. angalia pale Forodhani Zanzibar mpaka Aga Khan kaja kutupandia maua!(shame!)
Huyu anayaeitwa meya Wa jiji Bw Kimbisa anachojua ni kutembea na gari inayapeperusha bendera ya meya lakini haoni hata aibu mandhari ya Dar inavyotia kinyaa! Yaani tuseme na eposure yake yote kashindwa kuiga ha suala moja la kuboresha mji pamoja na vyanzo vyote vya mapato alivyonavyo?
Tunahitaji mabadiliko sasa ili tuweze kusonga mbele