nafikiri tatizo kubwa ni madereva ambao hawajitambui na hawathamini maisha yao wala abiria waliowabeba kwa kutokuzingatia sheria za barabarani. Ajali zitapungua tu pale ambapo madereva wataona umuhimu wa kufuata sheria wakiwa barabarani. Kila ajali inayotokea hasa hiz za mabasi lazima utasikia dereva alikuwa mwendo kasi, alikuwa anaovertake. Yaani kila siku story ni hizohizo.
kuna watu wanasema barabara mbovu ndio chanzo cha ajali, ni kweli barabara zetu mbovu lakini kama dereva anapita kwenye hiyo barabara mbovu kila siku, ina maana anajua wapi pabaya na wapi pazuri kwa hiyo anajua kuwa inatakiwa aendeshe gari kwa umakini mkubwa na speed ya wastani. Madereva vichaa ndio wale ambao wanajua kuwa barabara ni mbaya lakini anaendesha gari kama yupo kwenye mashindano ya formular one. Sehemu kuna kona haoni mbele lakini unakuta anaovertake tu. Hatuwezi kuepuka ajali hadi hawa vichaa waishe wote.
Nafikiri serikali na wadau wengine lazima wafike mahali waangalie namna na kushughulikia tatizo madereva wajinga na wasiofuata sheria za barabara. b