On a serious note: kutetea umachinga ni ushujaa?

Naafiki na mantiki ya wazo hili.
Hivi ni lini ndugu zetu wa Iringa walitoka kwenye kundi la The Big Four ya wazalishaji wakuu wa chakula nchini?

Cheap thinking and an equally cheap solution makes Mch Msigwa a novice katika Tanzania politics.
Vijana Iringa watakufa njaa kwa sababu hakuna political initiative ya kuwa galvanise into a production force.

Umachinga is basically a begging initiative.
Ni aibu.
 
Nimesoma thread nyingi sana za wadau, mengi yamesemwa na ni reflection halisi ya dhana ya umachinga na uchumi wetu. Bila shaka mnamkumbuka comrade mwananzuoni prof. Chachage. S. Chachage (late) aliwahi andika kitabu chake ''makuwadi wa soko huria'' hebu jaribuni kukitafuta na mkisome kwa umakini wana jamvi mtajua nini maana ya umachinga na hatma ya uchumi wa mlala hoi. To remove ignorance we start with conscious habit of learning. Ahsanten.
 

Hivi tukiwaondoa hao vijana mtaani, wataenda kulimaee. Au unadhani hawafanyi kilimo ksbu ya kufanya umachinga?
 
Erosion ya thinking katika safu ya wawakilishi wa wananchi sasa inaelekea kubaya-kwa maoni yangu!

Kwa mtu anayeelewa jinsi dhana nzima ya umachinga ilivyo asingeitetea kama mkombozi wa wananchi wasio na uwezo.
Thinking ni kwamba kwa vile barabara zipo, kwa hiyo kuna wateja barabarani, mtu hakodi cha kuweka tumboni.
Cheap thinking just as it is cheap attempt at appeasing political supporters.

Hebu tuichunguze dhana nzima ya umachinga.
Hii ni outlet of goods bila ya record za aina yoyote, kwa wasomi wa siasa ni kama kutetea anarchy, a political status quo ambayo hakuna control ya aina yoyote.

Kuna ukiukwaaji mkubwa wa kodi katika dhana hii ya umachinga, kwa vile records za bidhaa zilizoingizwa nchini, na ufuatiliaji wake wa kodi huwa hakuna.

Sasa kutetea hali hii inaleta wasiwasi kwa jamii yoyote ile.
Ni vema ikajulikana kuwa kama kuna kulipa kodi basi kila mtu asilipe ili iwe survival for the fittest.
Ni wazi kwa mtindo huu taifa linajinyonga lenyewe.

Tutofautishe kati ya wamachinga na dhana ya umachinga.

Wamachinga , originally kutoka Lindi ni kundi la vijana waliokosa kazi ya kuwapa ajira ya maana.

Hivyo basi ni vema wanasiasa wetu wakajikita katika kutatua tatizo la kuwapa vijana wetu matumainio ya maendeleo kwa kukuanzisha miradi yenye tija na manufaa kwa jamii.

Kutetea vijana kukaa vibarazani mwa wahindi au barabarani kuuza njugu na viatu hadi mitumba ni kujipatia umaarufu usio na tija. Ni kama kuvuta bangi ya kisiasana kutegemea matatizo yatapotea yenyewe.
pHakuna shortcut ya kutatua matatizo ya vijan wa nchi hii, na umachinga siyo solution.


UNAWEZA KUWA UNAJARIBU KUWAZA VEMA; LAKINI TULIFIKA VIPI HAPO? NA TUNAONDOKA VIPI HAPO BILA KUIUMIZA JAMII YA WATZ WANAOISHI KWA MTINDO HUO? JE KUNA MKAKATI WA KIELIMU, KISIASA NA KIJAMII KUTUTOA HAPO? JE NINI FOCUS YA KITAIFA KUKABILI HALII HII? AU NDO MAWAZO MEPESI KWA MAMBO MAZITO KIASI HIKI? JE JAMBO HILI HALIBEBI MUSTAKABALI WA AMANI YA NCHI HII? N.K. ANGALIZO KABLA HAUJAMPONDA MTU TAFAKARI KWANZA!!
 
Mkuu umejitahidi kuwa na analysis nzuri ya matatizo yanayowakabili wananchi wetu hudusan vijana wetu.

Hatuwezi kutofautisha matatizo ya kiuchumi na kijamii na tatizo kubwa linanoibuka la umachinga.

Kama matatizo yetu ni ya kiuchumi usioendelevu na kukosekana uzalishaji mali napata kigugumizi kufikiria kuwa moja ya suluhisho la ajira kwa vijana wetu ni umachinga.
Umachinga halisi ni retail street business kwa bidhaa kutoka kwa mapapa wa kibiashara wasiolipa kodi nchini, hilo ni wazi.
Mapapa hawa wa kibiashara wanajua fika kuwa wanasiasa wanawategemea sana wamachinga kwa umaarufu wa kisiasa.

Sasa kwa mwanasiasa makini kutetea umachinga ni sawa kabisa na kuinua huo ukwepaji wa kodi ulio wazi.
Mbaya zaidi ni wanasiasa wetu(tena wa kambi zote) kutolipa kipumbele tatizo hili ili litatuliwe huko huko linakozalishwa.
Hivi ni kwa nini watu hatufikirii kilimo, viwanda vidogo na hata usindikaji wa vyakula huko huko vijijini ili mali hiyo iuzwe kwa ujumla nje na ndani ya nchi.

mkuu Mimibaba umetoa kwa kweli analysis nzuri lakini conclusion yako ni "quick fix solution" isiyo endelevu.
Kuukubali umachinga ni kukubali kushindwa kuwahudumia vijana wetu.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…