masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,625
- 14,590
kwa sasa lazima watetewe maana angalau ni njia yao halali ya kujipatia riziki, umaachinga kwa ujumla ni zao la mfumo mbovu wa utawala hasa mfumo wa elimu na mfumo wa uchumi wa nchi, so hawa machinga ni victims tu hivo ni vema walindwe na wakti huo huo utafutwe mkakati wa muda mfupi na mrefu kuondoa tatizo hili.
Wengine wanatembea na visu viwili mchana kutwa!
Mkuu ielewe mada yenyewe, dhana ya umachinga na madhara yake.Mkuu kwanza ninashaka na thinking yako.
Jiulize Kariakoo na maduka mengine hata wanauuza vitu vya thamani kama simu hawatoi receipt?
Je mfumo wa serikali unawatafutaje na kuwachuklia hatua?
Pili kinachofanya machinga waendelee kuwepo kwenye miji ni msongamano wa magani na foleni kiasi kwamba unaenda mjini kwa lengo la kununua bidhaa husika chukulia hapa DSM kariakoo hakuna parking. Pale unapopata parking usalama wa gari ni mdogo sana. One of the solution ni kununua vitu hivyo ukiwa kwenye foleni (wamachinga).
Suala la Kodi ni Rahisi sana polisi/mgambo/TRA kusema kwamba machinga akikutwa hana receipt (genuine) ya bidhaa anazouza zinataifishwa pamoja na kifungo. kodi zitakusanywa za kutosha kupitia huko wanachukua bidhaa
Pili serikali inaweza kuanzisha eneo maalum la wamachinga kununua bidhaa zao kwa ajili ya kwenda kuuza hii ni pamoja na kusema ni bidhaa gani zinaruhusiwa kuuzwa kwenye barabara hizo n.k. Hapa kadi zitakusanywa tu kwa urahisi.
Tatizo ni Hatujawahi kusikia wamachinga wakifukuzwa Dodoma, Tanga, Morogoro, Tabora Shinyanga nk? Je huko hakuna Machinga?
Kama wapo TAFAKARI NA CHUKUA HATUA, Usiropoke tu
Serikali ya CCM imelifuga hili tatizo, vijana hawana ajira rasmi, wanahitaji kuishi kwa kufanya shughuli zilizopo UMACHINGA ili waishi, Bunge limetega Bil 3 kwenye bajeti hii, vijana wako takribani Mil 16, inamaana ni Tshs 187 kwa kila kijana, kwa mtaji huu unategemea Machinga wasiwepo, unategemea Msigwa asiwatetee wapiga kura wake?
Mkuu ielewe mada yenyewe, dhana ya umachinga na madhara yake.
Kutete mfumo huu usio na tija ni vile vile kutetea kutolipa kodi kwa wananchi wote.
Sioni mantiki ya mwakikishi wa wananchi kulalama kuwa fulani halipi kodi wakati anatetea kundi fulani la wasiolipa kodi.
Umasikini si kigezo, nchi yoyote iliyositawi kimaendeleo kulipa kodi sio option, bali suala ni kodi kiasi gani na mfumo mzima wa biashara.
Wengine wanatembea na visu viwili mchana kutwa!
Mkuu reality na philosophers wanatuambia kuwa you can not control history, but you can learn from it!Masopakyindi bhana ! Nimeamini wewe si Mtu wa aina ya Watz aisee, kwa hiyo tuwatose wamachinga kisa hawako kwenye Mfumo Rasmi ? Kweli nimeamini Aliyeshiba Hamjui mwenye njaa ! Hivi andiko lako lina Msukumo wa kisiasa ( kwa sababu Msigwa yumo ) ? Au lina msukumo wa kijamii au ni shibe tu uliyonayo ndiyo imekusukuma kuandika hivi ?