Omog amkubali straika wa DC Motema Pembe aliyetua Simba, sasa kumwaga wino Msimbazi

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
Hafidhi.jpg

Bosi wa benchi la ufundi la Simba, Mcameroon, Joseph Omog amevutiwa na kiwango cha mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Hafidhi Musa ambaye amejiunga nayo hivi karibuni akitokea Motema Pembe ya DR Congo.

Musa alionyesha kiwango cha juu katika mchezo alioitumikia Simba dhidi ya Nakuru All Stars ya Kenya jambo ambalo lilimfurahisha Omog na kujikuta akisema kuwa Hafidhi anajua.

Omog.JPG
Omog alisema amevutiwa na uwezo wa mchezaji huyo na ametoa maagizo ya kufanywa na uongozi juu ya mchezaji huyo.

“Tayari harakati za usajili zimeshaanza na hivi karibuni katika michuano ya SportPesa nimefanikiwa kuona baadhi ya wachezaji ambao nilivutiwa na uwezo wao, lakini aliyenivutia zaidi ni Hafidhi Musa yule mchezaji wetu aliyekuwa amevaa jezi namba 20.

“Ni mchezaji mzuri na ana vitu tofauti ukilinganisha na baadhi ya wachezaji wengine waliocheza mechi hiyo, kwa hiyo kuna maagizo nimeyatoa kwa uongozi dhidi yake, lakini pia nitahitaji kumuona zaidi pindi tutakapoanza mazoezi ya kujiandaa na ligi kuu msimu ujao,” alisema Omog.

Baada ya hivi karibuni kikosi hicho cha Simba kutupwa nje ya michuano ya SportPesa Super Cup wachezaji wa timu hiyo wamepewa mapumziko ya wiki tatu kabla ya kuanza tena maandalizi ya kujiandaa na michuano ya ligi kuu msimu ujao.

Chanzo: Champion
 
bado napata mashaka. mwaka jana tuliaminishwa kuwa mavugo na blagnon kuwa ndio mitambo ya mabao matokeo yake wanabaki na nyavu wanapiga nje. tena blagnon tuliambiwa na Hanspope kuwa atasaini mkataba kuwa akishindwa kufunga asilipwe lakini wapi. ushauri wangu mshahara wa Mavugo alipwe kichuya na blagnon alipwe Boco hao wageni wasepe sio kwa kukosa huko magoli. mchezaji mzuri kwanza huwa hajaribiwi pili sio wa kumtathimini kwa mechi moja akifluku utajuaje?
 
Bosi wa benchi la ufundi la Simba, Mcameroon, Joseph Omog amevutiwa na kiwango cha mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Hafidhi Musa ambaye amejiunga nayo hivi karibuni akitokea Motema Pembe ya DR Congo.

Musa alionyesha kiwango cha juu katika mchezo alioitumikia Simba dhidi ya Nakuru All Stars ya Kenya jambo ambalo lilimfurahisha Omog na kujikuta akisema kuwa Hafidhi anajua.

Omog alisema amevutiwa na uwezo wa mchezaji huyo na ametoa maagizo ya kufanywa na uongozi juu ya mchezaji huyo.

“Tayari harakati za usajili zimeshaanza na hivi karibuni katika michuano ya SportPesa nimefanikiwa kuona baadhi ya wachezaji ambao nilivutiwa na uwezo wao, lakini aliyenivutia zaidi ni Hafidhi Musa yule mchezaji wetu aliyekuwa amevaa jezi namba 20.

“Ni mchezaji mzuri na ana vitu tofauti ukilinganisha na baadhi ya wachezaji wengine waliocheza mechi hiyo, kwa hiyo kuna maagizo nimeyatoa kwa uongozi dhidi yake, lakini pia nitahitaji kumuona zaidi pindi tutakapoanza mazoezi ya kujiandaa na ligi kuu msimu ujao,” alisema Omog.

Baada ya hivi karibuni kikosi hicho cha Simba kutupwa nje ya michuano ya SportPesa Super Cup wachezaji wa timu hiyo wamepewa mapumziko ya wiki tatu kabla ya kuanza tena maandalizi ya kujiandaa na michuano ya ligi kuu msimu ujao.

Chanzo: Champion

Napingana na Omog na sina uhakika kama kweli Kocha wa hadhi yake na very Professional kabisa anaweza akamuangalia tu Mchezaji katika mechi moja na kusema ni mzuri. Hapa tusidanganyane kwani ninachojua technically kabisa ulimwenguni kote Kocha humuangalia Mchezaji mpya au ambaye anataka kumsajili angalau ndani ya mechi 3 mpaka 5 bahati mbaya huyu anayepigiwa chapuo kaonekana katika mechi moja tu halafu anasifiwa na hadi kupendekezwa asajiliwe.

Nikiwa kama Mdau mkubwa wa mpira wa miguu a.k.a Soka nasema kwamba sidanganyiki kijinga kijinga hivi na kama ni kweli kuwa kauli hii imetoka Kwake Kocha Omog mwenyewe basi kuanzia usiku huu wa Saa 6 na dakika moja kwa Saa za Afrika ya Mashariki naanza kumdharau na kumpuuza Kocha wa Simba SC Joseph Omog. Hata sisi wengine mpira tumeucheza na tunaujua vile vile na huyu Mchezaji si mzuri kihivyo ila najua Watu wanalazimishwa asajiliwe ili kama kawaida yao wapige 10% maisha yaendelee.

Karibuni tu nitaacha kufuatilia Soka la Bongo na Ligi yetu ya Madafu / VPL na kujikita tu zaidi na Timu zangu za Ulaya Liverpool FC ( Uingereza ), Bordeaux FC ( Ufaransa ), Bayern Leverkusen ( Ujerumani ), AC Milan ( Italia ), Ajax Amsterdam ( Uholanzi ), Celtic FC ( Uskochi ), Maccabi Haifa ( Israel ), FC Barcelona ( Uhispania ) na moja ya kutoka Ulaya ya Afrika ( Afrika ya Kusini ) Klabu ya Kaizer Chiefs.
 
Amog sio kocha wa kiwango cha Simba Sports Club.
Azam walimtema kwa kuonesha kiwango kidogo.

Sielewi alimsajiri vipi Blagnoni.
Mpaka sasa hana kikosi cha kwanza cha timu yake ya Simba.
Jambo hili limeighalimu timu ishindwe kuchukua kombe la ligi.
Nilimshanga sana kuwaacha wachezaji kama, Ndemla, Ajibu, Mkude, Kichuya, kuanza katika baadhi ya mechi muhimu, na kuwaanzisha akina Pastori, Blaginoni Mnyate na Yule wa mkopo toka Zesco.
Ni mzito wa kufanya Sub za haraka mchezaji anapoonyesha kuwa nje ya mchezo.
Hakika Amog ametunyima ubingwa msimu huu.

We Amog
Kocha ni lazina uwe na kikosi cha kwanza cha ushindi.
Mchezaji akiumia au kuchoka au kuwa nje ya mchezo ndo unafanya Sub ya haraka.

Wapenzi wa Simba wanaanza kikuchoka.
 
Mimi nilichek hii gemu jamii ni wakawaida tu ata apa bongo wapo wanacheza kwa kiwango kile ombi langu wasijaze nafas za wachezaj wa kigen kwa kuchukua wachezaj ambao apa bongo wapo kwa uwezo unaofanana hata yule beki kutoka Ryon ni wakawaida pia
 
Napingana na Omog na sina uhakika kama kweli Kocha wa hadhi yake na very Professional kabisa anaweza akamuangalia tu Mchezaji katika mechi moja na kusema ni mzuri. Hapa tusidanganyane kwani ninachojua technically kabisa ulimwenguni kote Kocha humuangalia Mchezaji mpya au ambaye anataka kumsajili angalau ndani ya mechi 3 mpaka 5 bahati mbaya huyu anayepigiwa chapuo kaonekana katika mechi moja tu halafu anasifiwa na hadi kupendekezwa asajiliwe.

Nikiwa kama Mdau mkubwa wa mpira wa miguu a.k.a Soka nasema kwamba sidanganyiki kijinga kijinga hivi na kama ni kweli kuwa kauli hii imetoka Kwake Kocha Omog mwenyewe basi kuanzia usiku huu wa Saa 6 na dakika moja kwa Saa za Afrika ya Mashariki naanza kumdharau na kumpuuza Kocha wa Simba SC Joseph Omog. Hata sisi wengine mpira tumeucheza na tunaujua vile vile na huyu Mchezaji si mzuri kihivyo ila najua Watu wanalazimishwa asajiliwe ili kama kawaida yao wapige 10% maisha yaendelee.

Karibuni tu nitaacha kufuatilia Soka la Bongo na Ligi yetu ya Madafu / VPL na kujikita tu zaidi na Timu zangu za Ulaya Liverpool FC ( Uingereza ), Bordeaux FC ( Ufaransa ), Bayern Leverkusen ( Ujerumani ), AC Milan ( Italia ), Ajax Amsterdam ( Uholanzi ), Celtic FC ( Uskochi ), Maccabi Haifa ( Israel ), FC Barcelona ( Uhispania ) na moja ya kutoka Ulaya ya Afrika ( Afrika ya Kusini ) Klabu ya Kaizer Chiefs.
Ferguson alimsajili Ronaldo baada ya kumuona kwenye mechi moja tu tena ya kirafiki alipokua akimgaragaza Garry Neville
 
Back
Top Bottom