Ombi/wazo kwa Serikali kuhusu hii kauli naomba iangaliwe upya kwa maslai ya Taifa

F35-Bomber

JF-Expert Member
Mar 18, 2017
1,348
1,066
(Applicants who have/were retired from the Public Service for whatever reason should not apply)
Habari zenu wakuu wa jamvi ni matumaini yangu kuwa wengi kama sio nyote ni wazima kwa nguvu za mueza.

Binafsi ninaomba nitumie pumzi hii ya leo kuiomba serikali kubadili kidogo mtazamo katika swala zima la ajira serikalini,

kwani katika moja ya masharti ya kuajiriwa serikalini wanasema muombaji wa nafasi hiyo asiwe alikwisha wahi kuajiliwa serikalini au kuacha au kufukuzwa au kustafishwa kwa namna yoyote ile.

Binasfi naona hii siyo sahihi kwani kuna mazingira mengi sana ya mtu kuacha,kuachishwa,kufukuzwa au kustaafishwa kazi.mimi ningeonelea kua ni busara kama mtu anasifa aombe kazi na aajiriwe kwani yeye ni mtanzania na na anaenda kutumikia watanzania

Hivi mnajua kua kuna mtu ni kijana bado ananguvu anaipenda nchi ila kisa amemzidi elimu bosi wake basi anafanyiwa figisufigisu na kwakua pia yeye ni binadamu basi anajikuta anaandika barua ya kuacha kazi serikalini ndani ya masaa 24 lakini kiekweli unakuta kijana ni mzalendo na anauwezo mzuri tuu wa kuisaidia serikali na hii ni angle moja tuu

Yapo matukio mengi tuu kama haya .hivyo basi naiomba serikali hii sikivu kutoa kipengele hicho ili watu wenye vyeti halali na ambao walikwisha tumika serikalini waweze pia kuajiriwa upya serikalini kama wanavyo vigezo na hawana makosa yoyote yale ya kijinai AKHSANTANI
 
Mfano aliyekuwa mganga mkuu wa hospitali ya mkoa wa Singida (mtanisahihisha kama nimekosea) aliposumbuliwa na mkuu wa mkoa akaona bora a ajiweke pembeni. Mtu kama huyu ni nongwa kuomba tena kazi?
 
Mkuu;
Nakupinga kwa mawili hivi; Kwanza huo ni mwanzo wa utumishi hewa. Uliacha ukaenda kulima, ukame unataka ukurudishe kazini?? No way and I say no way. Utakuja endelea na cheque namba ipi?? Mpya au ile ile ya zamani?? Acha wengine wenye vyeti hai na wabichi nao waonje keki letu.
Pili; Kwa jinsi ninavyo wafaham watu, endapo utaajiriwa upya kwenye kazi yako hiyo, kama uliondolewa kwa hofu ya ofisa wako mwenye cheti cha chini yako, leo ukienda ukamkuta na huklu sasa wewe umeomba kazi kubwa kuliko ile uliokuwa umepewa mwanzo. Huoni tiyari umeshaleta malumbano kazini na aliyekuwa boss wako??
Usiombe tena, endelea na hayo unayofanya sasa kwa ajili ya mlo wako.
Narudia tena; Acha wenzio nao waonje hiikeki hata kama ni kwa miezi 6 kabla hakujabuniwa mbinu nyingine ya kuwapunguza
 
Na Hayo ndiyo mawazo ninayo yapinga mimi mtu akiwa hayupo kazini anafutwa kwenye payroll pia cheki siyo msaafu kwamba haibadiliki watu wote wanafursa sawa na kua mtumishi hewa huo ni uzembe wa mtu mwingine siyo wewe,pia swala la chuki na bosi wako wazamani siyo always the case kwasababu kuna watu wanasifa kuajiliwa maeneo mbalimbali tofauti na eneo lake la awali nadhani nimejaribu kukujibu.
 
Kuwa huru kaka acha kupanic
Mtumishi yeyote anaweza omba kazi iwapo:-
Aliacha kazi kwa hiari yake bila kufukuzwa
Hana jinai yoyote
Anasifa linganishi hasa umri.
Jambo la msingi hapa ni kuwa cheque bamba yako itatumika kukulipa tena ukiajiriwa serikalini kuepusha double payment kwani unatakiwa kuwa wazi unapoomba kazi kuwa uliajiriwa na ikibidi onesha document zako kama sehemu ya CV yako kwa uhakika zaidi ikiwamo na cheque namba.
 
Ni wazo zuri. Tena ikiwezekana mtu anaajiriwa anafanya kazi miaka kumi, halafu baada analazimishwa kustaafu na kukaa nje ya ajira ya serikali kwa miaka kumi, ndipo arudishwe tena kama atakuwa anataka tena.
 
Na Hayo ndiyo mawazo ninayo yapinga mimi mtu akiwa hayupo kazini anafutwa kwenye payroll pia cheki siyo msaafu kwamba haibadiliki watu wote wanafursa sawa na kua mtumishi hewa huo ni uzembe wa mtu mwingine siyo wewe,pia swala la chuki na bosi wako wazamani siyo always the case kwasababu kuna watu wanasifa kuajiliwa maeneo mbalimbali tofauti na eneo lake la awali nadhani nimejaribu kukujibu.

Aksante kwa kujaribu ila, jua kwamba unatakiwa uoneshe vyeti vile halali, vya jina lako halali ambalo ulikuwa unalitumia enzi hizo. Hapo ndio utajua kuwa system huwa haimfuti mtu kwenye kumbukumbu zake. Utakapo weka jina la; Mr. Chakupewa bin Umepatwa, Jinsia M, kuzaliwa 1947, Mkoa, Songea tiyari limashine lile litasema, jamaa yupo kwenye system. Acha wengine wapya nao waje kujionjea hili likeki jaman.
 
HICHI NDICHO NINACHOKIZUNGUMZIA KUWA KWENYE SYSTEM SIYO DHAMBI KIASI HICHO NA HATA MTU UKIOMBA TENA AJIRA SERIKALINI ETI UKOSE KISA TU ULIWAHI KUAJIRIWA SERIKALINI NA HII NDIYO HOJA YANGU HAPA.
 
Back
Top Bottom