TEKNOLOJIA
JF-Expert Member
- Jan 6, 2014
- 4,305
- 2,563
CCM ndio wamemshagua mgombea wao wa urais,Dr John Pombe Magufuli,Hakuna asiyemjua Magufuli kwa uchapa kazi wake,Watanzania wengi wanamkubali sana.
Nawashauri UKAWA,mtakapoanza kampeni za urais ni vyema mkalenga katika changamoto zinazowakabili wananchi kila siku. Kampeni yenu ijikite katika namna mtakavyompunguzia gharama za maisha mwananchi wa kawaida,kwa kumpunguzia mzigo wa kodi.Ishambulieni CCM kama mfumo wa ulioshindwa kuifikisha nchi pale ilipotarajiwa,na namna gani nchi inahitaji mfumo mpya utakaowaharakishia maendeleo wananchi na nchi kwa ujumla.
Udhaifu mkubwa wa Dr Magufuli upo katika haiba yake ya ubabe na ile ya kutoambilika,meli ya uvuvi inaweza ikawa case study nzuri sana katika kuonyesha hasara za kuwa na viongozi wa aina hiyo kwa taifa.
Achaneni kabisa na ufisadi,mkienda na mkakati huo mjue mtashindwa,Dr Magufuli hawezi kuchafuka kwa kashfa za ufisadi kwasababu wananchi wana imani naye sana.Kazi kubwa itakuwa huko kanda ya ziwa,UKAWA mjipange hasa.