Pia kuwe na mawakala mbadala kama sheria ya uchaguzi ya 2010 inavyosema ili Chadema watapoona mwenendo wa wakala sio mzuri basi anabadilishwa. Pia wapeane zamu, yaani ikifika saa tisa kabla ya kituo kufungwa saa kumi wakala aliyeanza asubuhi anaondoka na yule mbadala anaingia ili kuongeza ufanisi kwenye zoezi la kuhesabu kura na kulinda matokeo na kuweza kukaa mpaka anaweka sahihi na kuondoka na nakala ya matokeo (kila wakala au wakala mbadala lazima awakilishe nakala ya matokeo kwenye chama chake, hii itasaidia kuonesha kuwa wakala amekuwapo mpaka mwisho). Nasema hivi kwa sababu zoezi linaweza kwenda mpaka saa nane au tisa za usiku.
Pia mawakala wasikubali vyakula kutoka kwa watu wengine, kwani wanaweza kujikuta wakati wa kuhesabu kura na kubandika matokeo wanapiga usingizi wa kufa mtu. Wachukue maji ya kilimanjaro - chupa kubwa, biskuti za glucose za kutosha, na simu zao ziwe na vocha za kutosha, wapige picha matukio yote ya kutatanisha kama simu zina kamera au ata kurekodi!