Ombi kwa Rais Magufuli, Peleka fedha za Maendeleo ya Reli kwenye Madawati

Usedcountrynewpipo

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
3,636
2,725
Mh Magufuli,wewe ndio umeshakuwa Raisi wa nchi hii kwa kipindi cha miaka mitano iwapo Mwenyezi Mungu atakuweka hai kwa kipindi hiki. Kwa hiyo kama mwananchi wa nchi hii ninawajibika kukupa kila aina ya support kuhakikisha taifa linasonga mbele.

Hivi karibuni nilipokuwa naainisha aina za kodi tunazotozwa wananchi, nikaona kuna kodi ya maendeleo ya reli (Railway development levy) ambazo ni pesa tunachangia tunapo agiza bidhaa mbali mbali.

Sasa kulingana na umuhimu (urgency) iliyoko katika sekta ya elimu ya wanafaunzi kukaa chini au kwenye madarasa yaliyo chini kabisa ya kiwango, na kwa kuzingatia kuwa hakuna uharaka wa miundombinu ya reli ukilinganisha na uharaka ulioko kwenye sekta ya elimu, badala ya kupeleke hayo makusanyo kwenye reli ambapo huko nyuma wajanja walipiga dili na kuletea mabehewa mabovu, ninakushauri fedha hizo uzielekeze kwenye kuchonga madawati na kuboresha miundombinu ya elimu kama vyoo, madawati, majengo n.k kwa miaka mingine mitatu...

Then mambo yakiwa poa kwenye sekta ya elimu ndipo makusanyo hayo utayarudisha tena kwenye sekta ya miundo mbinu.

Ukifanya hivyo kwa kutangaza tenda kwa mafundi seremala wa chini angalau kila mmoja akapata tenda ya kuchonga madawati mia au kwa shule moja, utakuwa pia umetoa mchango mkubwa kwenye suala la ajira kuliko hizi hela ambazo mabehewa, reli n.k zinatoka nje ya nchi hivyo kuchangia kwenye ajira za wenzetu.

Natumaini utalifanyia kazi swala hili na pia ninaomba watumishi wako wakufikishie ombi hili iwapo wewe binafsi hautaona.

Mods naomba mhakikishe ombi hili linafika mahala husika...
Wako, Mjenga Nchi ni Mwananchi aka Used country new people...
 
naona sasa mmeanza kuuona ukweli maana mtu ulikua ukisema unaambiwa we mpinzani bahati nzuri ukweli unaanza kujidhihirisha
 
naona sasa mmeanza kuuona ukweli maana mtu ulikua ukisema unaambiwa we mpinzani bahati nzuri ukweli unaanza kujidhihirisha


uhaba wa madawati ni changamoto kwa wanafunzi hasa wa elimu ya msingi.
viongozi waongeze juhudi kutatua hili.
 
Back
Top Bottom