Kuwepo kwa umaskini na magonjwa mbalimbali imedaiwa ni vyanjo vya ongezeko la ombaomba jijini Dar es Salaam.
Idadi ya ombaomba hapa nchini imedaiwa kuongezeka siku hadi siku, huku baadhi yao wakitoa sababu za kushindwa kulipia gharama za matibabu.
Akizungumza leo Jumatatu, Julai 31 Hussein Juma amesema kilichomsababisha yeye kuwa ombaomba ni umaskini baada ya kushindwa kupata elimu.
"Nahitaji elimu ilibidi niombe baada ya kutelekezwa na baba na hivyo kuamua kuishi na mama ambaye hana kipato chochote kwa sasa," amesema Juma.
Pia, amesema mama yake anahitaji msaada pamoja na wadogo zake wawili ambao wana umri mdogo.
"Nikipata mtu wa kumsaidia mama yangu na pia kunisomesha nitafurahi na nitaacha kuomba," amesema Juma.
Nilipomuuliza kuhusu mama yake anafanya nini kumsaidia alijibu kwa sasa mama yake anawaangalia wadogo zake wawili hivyo inabidi amsaidie.
Pia, Salum John amesema ni mzawa wa Mtwara ila alikuja Dar es Saam kwa ajili ya matibabu baada ya kuona anatibiwa pasipo kupata nafuu.
" Mpaka sasa sijaweza kumudu gharama za kufanya vipimo vikubwa ili kujua ni kwa nini kidonda nilichonacho mguuni hakiponi hivyo niliamua kuomba ili niweze kupata fedha za matibabu na pia za kujikimu kimaisha kwani sina ndugu," amesema John.
Omba omba hawatakaa waishe mpaka keki ya taifa inufaishe kila mtu kwa usawa kuanzia elimu, afya, makazi na kila kitu cha msingi kama wenzenu Brunei, Qatar
Omba omba hawatakaa waishe mpaka keki ya taifa inufaishe kila mtu kwa usawa kuanzia elimu, afya, makazi na kila kitu cha msingi kama wenzenu Brunei, Qatar
Fanya kufika alipohifadhiwa seth sing na rugemarila wanaweza kukupa direction kwa urahisi zaidi.
Ukishindwa kabisa muone macho ya cobra anaweza kukusaidia