Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,428
OLIVER SEMUGURUKA APONGEZA USHINDI WA MADIWANI WA VITI MAALUM WILAYA ZA MKOA WA KAGERA
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kagera, Mhe. Oliver Daniel Semuguruka ametoa pongezi za dhati kwa Madiwani wa Viti Maalum kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Kagera kutokana na ushindi waliopata kwenye uchaguzi uliofanyika tarehe 20 Julai, 2025
"Nawapongeza kwa dhati Madiwani wetu wote wa Viti Maalum mliochaguliwa siku ya Jana tarehe 20 Julai 2025, kupitia mikutano mikuu ya UWT Wilaya zote za Mkoa wa Kagera" - Mhe. Oliver Semuguruka
"Hongereni kwa kuaminiwa na Chama Cha Mapinduzi pamoja na wajumbe wote wa Mikutano hiyo. Naamini mtawawakilisha Wanawake wote kwa ujasiri, kwa mshikamano, na kwa ufanisi mkubwa" - Mhe. Oliver Semuguruka
"Lakini pia nawapongeza na wale wote ambao kura hazikutosha kwa awamu hii. Msikate tamaa maana Mwenyezi Mungu anajibu kwa wakati naamini ipo siku mtafanikiwa!" - Mhe. Oliver Semuguruka
Ajenda yetu ni Ile Ile, Oktoba Tunatiki✅
Kazi na Utu, Tunasonga Mbele 🙏
©Oliver Daniel Semuguruka
#Twiga