Ole Medeye, Guninita wamshukia Membe kama mwewe

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,786
Siku moja baada ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kusema akionana na waliokuwa wanachama wa CCM na kuhamia upinzani anajisikia kichefuchefu, waliokuwa makada wa chama hicho wamemshukia kwa kauli yake hiyo.

Membe alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akitoa maoni yake kuhusu makada waliohama na kusisitiza kuwa wasipokewe endapo watataka kurudi.

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye ambaye alitimkia Chadema, alisema kama angesikia maneno hayo kwa mtu mwingine asingeshangaa, lakini siyo kwa Membe.

Mbunge huyo wa zamani wa Arumeru – Magharibi, alisema Membe anapata masilahi yake kwa kutambulika kama waziri mstaafu na wakati anaapa kuwa katika nafasi hiyo alitumia Katiba ambayo hivi sasa kwa kupinga yaliyomo ikiwamo uhuru wa mtu kujiunga na chama chochote cha siasa, anakosea.

Medeye alisema kwa kauli hiyo, Membe hana haki ya kugombea nafasi yoyote ya siasa kwa sababu haamini katika vyama vingi wakati Taifa linaendeshwa kwa Katiba inayokubali suala hilo.

Alisema hata kauli ya Membe ya kutounga mkono uchaguzi kurudiwa Zanzibar akitaka kufanyiwa kazi kasoro chache ni ya kinafiki kwa sababu ameonyesha kutopenda upinzani.

“Hana msimamo hazungumzi vitu kutoka moyoni, kama kweli anakubali vyama vingi na ana uchungu na kinachoendelea Zanzibar, kwa kuwa bado ni mjumbe wa Nec (Halmashauri Kuu ya CCM), angemuomba mwenyekiti wake aitishe mkutano mkuu lijadiliwe hilo na atoe anachokiamini, hakufanya hivyo kwa sababu hakubali vyama vingi, hataki mabadiliko katika siasa anayoitumikia, ”
alisema Medeye.

Aliyekuwa kada mkongwe wa CCM, Kingunge Ngombale Mwiru alisema hawezi kujibizana na watu kwani anajua anachofanya.

Alisema anayo mawazo huru na akitaka kuzungumza jambo lolote atafanya hivyo kwa utashi wake na siyo kujibizana na watu waliozungumza kwa utashi wao.

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita alisema anamheshimu Membe kwa sababu amefanya naye kazi katika chama hicho tawala na kumshauri siku nyingine anapozungumza mambo kama hayo asiegemee upande mmoja.

Alisema licha ya kuwa hayo ni mawazo yake na kila mtu ana uhuru wa kuwaza na kusema anachotaka, alipaswa apime anazungumza nini na kwa manufaa ya nani.

Guninita alisema Katiba ya nchi inamruhusu mtu kuhama chama hata mara 10 alimradi huko anakokwenda atapata vitu muhimu ikiwamo malengo yake binafsi, ya chama husika na mafanikio ya Taifa.

Alisema haikuandikwa ni lazima abaki sehemu anayoamini hana malengo nayo, au asihame kutoka chama kimoja ama kingine
 
membe ni janga hata kaa amsahau Lowasa naona bado ana hasira na magu hajampa kazi
Huyu haeleweki sasa, Mara anaikosoa ccm mara anaukandia upinzani, sijui tumuweke kwenye group gani? maana ni heri mtu aliyekaa kimya anaweza kuonekana yupo neutral
 
Membe hawamuwezi anazungumza vitu ambavyo vitakuja kuonekana baadae .ila kwa sasa watu hawajui hilo .kwanuni mtu akitoamaoni yake anaonekana msaliti .?
 
Membe hawamuwezi anazungumza vitu ambavyo vitakuja kuonekana baadae .ila kwa sasa watu hawajui hilo .kwanuni mtu akitoamaoni yake anaonekana msaliti .?
hicho kichefuchefu chake kitaonekana baadaye wapi ? halafu mbona alijiapiza kuwa rais , kiko wapi sasa ?
 
Hakuna Kitu Kama Hicho, Hana Nafasi Ktk TISS Ya Sasa Na Hata Yeye Analijua Hilo.
Hata wewe unajua kuwa huwa hawaachi kazi,membe limebobea katika character assassination,na kazi yake imeonekana mzee yu taabani kabisa kuliko wakati wowote.ndio maana kadandia ya zanzibar ili aanze kupamba vichwa vya habari
 
Hata wewe unajua kuwa huwa hawaachi kazi,membe limebobea katika character assassination,na kazi yake imeonekana mzee yu taabani kabisa kuliko wakati wowote.ndio maana kadandia ya zanzibar ili aanze kupamba vichwa vya habari

Labda Kwa Kukusaidia Tu Ni Kwamba Nguvu Yake Ya 100% Ya KIJASUSI Iliishia Mwaka 2005 Na Baada Ya Hapo " Chinga Boy " Amebaki Kuwa " KIDAMPA " Na Hana Anachokijua Kwa Sasa Ndani Ya IDARA Na Hawezi Hata KUTHUBUTU Kuyajua. Kuhusu Kusema Kuwa Huwa HAWASTAAFU Upo Sahihi Ila Ukumbuke Tu Kuwa Hata Kama Wakiwa Wanapeleka TAARIFA Zao Za KIJASUSI Bado Zitapitia Ktk Mikono Ya MAAFISA WAKUU VIONGOZI Kwa Kuchujwa Ili Kupima UHAKIKA Wake Na Usishangae Hata Kile Anachokipeleka Nacho KIKATUPWA Vile Vile. Mwisho Usije Ukasahau Kuwa Hata Kama Umewahi Kuwa Afisa Mwandamizi MSTAAFU Lakini UKISTAAFU Bado Pia Utakuwa Unafuatiliwa Tena KUNAKOTUKUKA Ili Kuweza Kujulikana Unafanya Nini Na Unaweza Ukawa THREAT Kiasi Gani Kwa Idara Hivyo UPOPOMA Wote Wa " Chinga Boy " Unajulikana Na " Eagle Wing House " Siku Nyingi Mno Na Hakuna ATAKACHOFANIKIWA Nacho. Mkuu Hilo Neno " INTELLIGENCE " Lina Maana Pana Na Linabeba UZITO Wote Ktk Ustawi Wa Nchi Na Kulinda Mipaka Yake Iwe Kwa Ndani au Nje Ya Nchi. Na Hata Hivyo Siku Zote Wale Ambao Huwa Ni Tishio Ni Hasa Hasa Wale WAKURUGENZI WAKUU Kama DG, DIO, DEO Na Yule Wa PSU Ila Si Kwa Watu Waliokuwa Ni Wakuu Tu Wa Vitengo Kama Alichokuwa Nacho " Chinga Boy " Naomba Niishie Hapa Tafadhali!
 
Kwa kuhama tuu chama mtu unamwona mwenzio kichefuchefu!! Kwakweli sijawai mwona binadamu mwenzangu nkaskia kichefuchefu kwa uamuzi Wake halali wa imani ama itikadi zisizovunja katiba.
Huyu anaendaga kanisani kweli,mbona anachuki za ki mpinga kristo...
mtu amwonae mwenzie kichefuchefu ni rahisi "kumwondoa " ili abaki na amani.
Viongozi wa hulka hizi ni hatari na si mfano wa kuigwa kabisa.
najiuliza,i
mkristo gani huyu?
Mwana diplomasia gani huyu?
Msomi gani huyu? Na
kiongozi gani huyu?
Niliwahi kuvutiwa na huyu mh. enzi akiwa waziri lakini nimepata mashaka,mheshimiwa kawa mhishiwa.
 
Back
Top Bottom