OKWI agoma kuongeza Mkataba Simba

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2011
Posts
4,225
Reaction score
869
Jamani nimepata taarifa muda mfupi uliopoita eti kwamba yule mchezaji hatari wa simba Emmanuel Okwi amekataa kuongeza mkata mwingine wa kuichezea Simba kutokana na mkataba wake kubakiza miezi sita ya kuichezea klabu hiyo?naomba nifahamu hili jambo kwa sababu linanichanganya sana.
 
Habari hii umepata wapi? Acheni kulisikiliza maneno ya kwenye vikao vya kahawa. Okwi mwenyewe atasaini mkataba mpya ila tatizo alilosema ambalo linampa tatizo hadi sasa hajasaini anadai kuna mtu anataka ule mgao wa dola 50,000 za signing fee jambo ambalo hakubaliani nalo. Binafsi namuunga mkono cz anajitambua.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Roho inakuuma nini sasa na wewe unajulikana ni wa upande wa pili, ngoma sio yako vibwaya vya nini? Umbea kwa mtoto wa kiume haufai.
 
Roho inakuuma nini sasa na wewe unajulikana ni wa upande wa pili, ngoma sio yako vibwaya vya nini? Umbea kwa mtoto wa kiume haufai.
hao wa Upande wapili wanajulikana mkuu; pesa za kununulia wachezaji wakali hawana, wanasubiri kudandia-dandia tu, wanaomba Okwi asisaini mkataba ili wao wa mpate bure kama siyo bei cheee.
 
Roho inakuuma nini sasa na wewe unajulikana ni wa upande wa pili, ngoma sio yako vibwaya vya nini? Umbea kwa mtoto wa kiume haufai.

Masuke nakuheshimu sana sipendi matusi,lakini pili kumbuka mi ni mwanamichezo kitu kama hicho si vibaya nikafahamu na ndo maana nimeuliza.
 
Mkuu haya maneno ndio nayataka ili niweze kujua endelea kumiminika kwa undanbi zaidi inaonekana una vitu juu ya jambo hili.
 
Masuke nakuheshimu sana sipendi matusi,lakini pili kumbuka mi ni mwanamichezo kitu kama hicho si vibaya nikafahamu na ndo maana nimeuliza.
Mkuu wabheja sana hata mimi nakuheshimu pia na tuendelee kuheshimiana lakini unapoleta habari kama hizi na huna uhakika nazo kwa nini usiweke kama tetesi maana ulivyoandika ni kama vile una uhakika na habari yenyewe, unajua kuna baadhi ya mashabiki wanapenda timu zao kupitiliza sasa mkuu unapoandika habari kama hii ambayo huna uhakika nayo unaweza kujikuta unaua bila kukusudia kumbe na habari yenyewe isiwe ya kweli.

Bahati nzuri wewe unaonekana ni homeboy, kule kwetu kuna utani wa jadi unajulikana kama 'bapugu' kuna bapugu wengine anaweza akakwambia baba yako ni mgonjwa wa kufa na kama wewe una matatizo ya moyo unaweza jikuta unatangulia, hivyo mkuu mimi nilitaka niweke angalizo habari kama hizo zinaumiza wengine ni afadhali basi ungekuwa na uhakika nayo. Kwa huu mchango wangu nadhani tutaendelea kuheshimiana.
 
Hivi bado kuna Watu wanaweza kusononeka kwa Okwi kuto'sign? Okwi alikuwa mwaka jn bwana,mwaka huu Okwi ni kama Tegete wetu.
 
kumbea ni umbea bwana... aondoke tu ili muache kuchonga..
 
Mkosi ukishatua mahali kila kitu kitaharibika!
 
Kama hawaoni umuhimu wako,okwi njoo mitaa ya twiga na jangwani ukutane na wachezaji wa hadhi yako.
 
Hivi bado kuna Watu wanaweza kusononeka kwa Okwi kuto'sign? Okwi alikuwa mwaka jn bwana,mwaka huu Okwi ni kama Tegete wetu.
Tafadhali,mpe heshima yake Tegete wetu!
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…