Okoa tanzania 1.

Okoa tanzania 1.

Jrafiki

Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
75
Reaction score
15
Ni ukurasa wa kazi na tenda na heading inasomeka OKOA TANZANIA, huu ni mfululizo wa mawazo na mitazamo katika kujadili mambo mbalibali yananayohusu taifa letu (Nyote mwakaribishwa). Naamini hapa ni sehemu sahihi na tunaweza kusaidiana kwa pamoja kimawazo kwa kuwa tupo watu wa taaluma mbalimbali na pia uzoefu mkubwa katika utendaji kazi na isitoshe Watanzanaia wote ni ndugu n.k.
Ningependa tuanze na haya MAKAMPUNI YA KUTAFUTIA WATU AJIRA ( Recruiting Agency).
Ni mara nyingi nimekuwa nikitafakari na pia kupitia sheria ya ajira na mahusiano kazini lakini nimekuwa sielewi baadhi ya mambo yanavyoendeshwa katika taifa letu (sijui kama ni mapungufu ya kisheria ama la!). Hivi, ningependa tujuzane;
1. Haya makampuni yanasajirwa na nani?
2. Yanasajiliwa kwa sheria zipi na chini ya kifungu namba ngapi?
3. Yanapopewa usajiri ni nini majukumu yake?. Hili swali laweza kuwa na majibu mapana sana ila sehemu ambayoningependa tuilenge katika majibu ni je, yanaruhusiwa kuajiri ( Employment)? Au yanaruhusiwa kutafuta wafanyakazi tu (recruiting process) na kisha suala la kuajiri kuachwa kwa kampuni au taasisi inayohitaji wafanyakazi? Au yanaruhusiwa kufanya yote kwa pamoja?
4. Kama yanaruhusiwa kuajiri, hawa wanaowapa kibari cha kuajiri WANAWAPA KIBARI CHA KUAJIRI KWA KAZI ZIPI WALIZOKUWA NAZO WAO?
Kwa nyongeza katika hilo,
a. Je, wanapima uwezo wao kifedha katika kuajiri?,
b. wanawafutilia masuala yao katika utendaji (monitoring and regulating) au wakishawapa usajiri basi imeshatoka recruiting agency kuachwa huru kufanya kile wanachokitaka?
Baada ya kuyajua hayo tuelekee katikakujuzana sheria inasemaje kuhusu kutoa kazi za mikataba?
Hivi sheria inasemaje kuhusu mwajiri kumpa mwajiriwa mkataba wa kazi wa muda wa miezi mitatu mitatu mara kwa mara bila kumpatia ajira ya kudumu?
maana kuna kampuni flani (recruiting agency) inaajiri na kuwapa vijana mikataba ya miezi mitatu mitatu katika kipindi chote cha ajira zao pasipo kuwapa mkataba wa kudumu,mfano zaidi ya miaka 2,3,4 mpaka mwajiriwa atakapoacha mwenyewe.
Haya mambo ni vema yafahamike katika umma, inaeleweka wazi kuwa kwa sasa kuna idadi kubwa sana ya vijana wanaomaliza elimu ya vyuo vikuu na wengine hawakufika lakini wanautaalaamu wa kazi flani kisha kukosa ajira, sitaki kwenda kiundani juu ya hili lakini haya makampuni ya kutafutia watu ajira baadhi yao yanaonekana wazi kutumia hali hii VIBAYA SANA katika KUNYONYA, KUKANDAMIZA na KUONEA vijana hawa kwa maslahi yao binafsi kisa tu AJIRA IMEKUWA BIDHAA ADIMU.
Wanasheria, Viongozi husika wa kitaifa katika masuala haya( Waziri wa kazi na viongozi wengine ndani ya wizara), Wasomi, Wanaharakati, Wazalendo na watu mbalimbali wenye ufahamu juu ya masuala haya naomba mtoe ufafanuzi juu ya masuala/maswali hayo manne juu.
Kwa kumalizia tu, nini lengo la kuibua hoja hii,
Kubwa ni kuijenga nchi yetu na kutumia fulsa zilizopo ndani kwa manufaa yetu wenyewe, kabla hatujaangalia wawekezaji wapya. TUJIULIZE, JE TULICHOKUWA NACHO (KILICHOWEKEZWA TAYARI KWA SASA) KINATUSAIDIA?, TUNAKITUMIA VIZURI? Haya mataasisi makubwa ya fedha, kampuni kubwa ya mawasiliano na makampuni ya bidhaa mbalimali kama nayo yanashirikiana na makampuni ya kutafutia watu ajira katika kutoa mikataba ya kazi ya KINYONYAJI NA UONEVU kwa vijana wanaotegemea ajira toka katika wawekezaji hawa, je vijana sasa wafanye nini? Wata’GROW’ saa ngapi? Nini faida ya wao kuwekeza hapa? Wanawekeza ili Wawanyonye Watanzania?
Pili tunaelewa fika kuwa idadi ya vijana wanaopata fursa ya kuitumikia Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni CHACHE MNO ukilinganisha na wahitimu wa vyuo katika kada mbalimbali kuanzia ngazi ya cheti, diploma, degree na postgraduate degree. Kwa mantiki hiyo sekta binafsi ndiyo zimekuwa na nafasi kubwa katika kuwaajiri wanataaluma hao, kama ni hivyo basi hatuna budi kuziwekea mazingira mazuri kisheria na usimamizi mzuri sekta hizi binafsi ili kuleta tija katika mchango wao wa kuwekeza nyumbani Tanzania hasa katika masuala ya utoaji ajira.
OKOA VIJANA , OKOA TANZANIA , JENGA TAIFA IMARA LA UADIRIFU KIUTENDAJI, IJENGE TANZANIA.
 
Back
Top Bottom