Okoa gearbox ya gari yako sasa

Okoa gearbox ya gari yako sasa

Joined
Jan 20, 2026
Posts
78
Reaction score
108
DALILI 7 ZINAZOASHIRIA TRANSMISSION ( GEARBOX ) YA GARI YAKO IKO HATARINI KUFA.
Transmission yako mara nyingi hutoa ishara za tahadhari mapema kabla ya kuharibika kabisa. Haswa katika magari yenye Automatic transmissioni ila kwa namna moja ama nyingine kwa wengi huwa ni ngumu kuelewa hadi pale ambapo tatizo linakua kubwa zaidi,

Sasa leo tunakuwekea hapa Redflags 7 ambazo ukiona hata moja katika gari yako basi chukua jitihada za haraka na mapema kabisa kwenye kuiokoa kabla haijafa mazima.

1. Kuruka Gear/s :
Ikiwa utaihisi gari yako kwamba kwa namna fulani inakua na hali ya kwamba unapokua kwenye mwendo inaunguruma tu lakini kasi haiongezeki kama ambavyo inapaswa kuwa. Ama kuihisi kwamba inapoteza nguvu punde inapokua inabadili gears haswa ukiwa kwenye maeneo yenye muinuko

2. Kelele zisizo za kawaida :
Ikiwa katika wakati wowote utahisi kwamba gari yako inatoa Sauti za ajabu ajabu kama vile Sauti za kulalamika, ku-unguruma, kugongana vyuma , au kusaga, hasa wakati wa kubadilisha gia, mara nyingi hii inaashiria kwamba kuna kiwango kidogo mno cha oil kwenye transmission yako au sehemu kwenye transmission yako zilizochakaa

3. Harufu ya kuungua :
Ikiwa kwa wakati fulani utahisi gari yako kwa namna fulani inatoa harufu ya kitu ambacho kinaumgua , hii inaashiria kwamba , hali ya joto kwenye geabox transmission yako imeongezeka ( overheating ) na kuashiria baadhi ya vitu vya muhimu vimeanza kuharibika

4. Dalili ya vitu kuvuja ;
Chungulia chini ya gari yako kwa upande wa mbele, ikiwa utaona kuna vitu ( mafuta / oil ) ambavyo vinavuja mfano wa rangi nyekundu ama brown hii huashiria kwamba oil ya gearbok inavuja kitu ambacho kinasababisha umwagikaji na upungufu wake.

5. Taa ya Dashboard
Jaribu kuzingatia pia dashboard yako, kwasababu kwa magari haya ya kisasa yenye kutumia umeme sana huwa lazima computer ya gari yako inapo ditect tatizo basi hutoa viashiria kwenye dashboard yako kwa mara nyingi kuwasha taa za alama hivyo inakupasa kuwa makini na alama yeyote inayojitokeza kwenye dashboard yako

6. Kuchelewa kuingiza / kubadilisha gear:
Ikiwa labda kwa namna moja au nyingine, wakati unaendesha gari yako unaihisi kwa namna fulani, either kutoweza kubadili gears kwa wakati, kuchelewa kuzibadili kulingana na mwendo husika au eneo husika - basi fahamu tayari huko panataka kuumana.

7. Gears kutoingia kabisa;
Pale ambapo na gears zinapogoma kabisa kwenye kuingia - tambua wazi kabisa tayari huko kumeshaumana
vibaya mno

SULUHISHO:
1. Angalia kiwango cha oil yako ya gearbox
Haswa haswa rangi yake na harufu yake , ikiwa utakuta.
Hakikisha kwamba ina rangi nyekundu ama pink yenye wekundu fulani sambamba na ka harufu fulani ka kuvutia ( hainuki moshi wala vyuma )

2. Nenda kwa fundi / garage:
Hakikisha kwamba Usicheleweshe; kwa sababu dalili hizi zinaweza kusababisha matatizo makubwa na ya gharama kubwa za ufundi/ matengenezo kwa hivo punde tu uonapo dalili yeyote kati ya hizi 7 hapo juu, basi jitahidi kumuona fundi mwenye weledi ama kupeleka gari yako kwenye garage zenye hadhi nzuri waweze kuikagua na kutibu tatizo.

Tunajihusisha na elimu kuhusiana na magari aina zote , uuzaji na uagizaji pia wa aina zote za magari
Kwa kulipia chini ya asilimia 100% baada ya gari lako kufika (hauna haja ya kulipa kabla gari haijafika)

TUPO ARUSHA KALOLENI KWENYE JENGO LA CONDO HOTEL LILILOPO MKABALA NA SHALOM CHURCH

OFFICE NUMBER 016 GROUND FLOOR

☎️
: +255797113153

... " Good Morning, the awaited Joy has came! "...
 
Iwapo gear box imeharibika na kutoa vipande vya vyuma wakati wa kumwaga oil,inatengenezeka?
 

Attachments

  • DSC_0008.JPG
    DSC_0008.JPG
    769 KB · Views: 1
Back
Top Bottom