Ogopeni wapiga dili kubwa, ya Lugumi yataisha hivi....

Jumong S

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
7,377
10,641
Wakuu,

Wapiga dili wengi huwaza kilomita maelfu mbele kabla ya kupiga dili. Yaani hawa jamaa hujipanga mapema na huwa wanajua madili ipo siku yatabumbuluka na wanaandaa namna ya kujinasua ikiwa yatawakuta. Mchezo wote huucheza katika mikataba. Hapa jamaa hujiandaa kwa mikataba itakayowalinda pindi wakifikishwa mahakamani. Chukulia mfano ndg Rugemalila, huyu machoni kwa watanzania alionekana kaiba kijanja, achilia mbali yule Singasinga, ila mikataba iliwalinda na wakafikia hatua kuishtaki serikali na kudai fidia.

Yaani uliyemuona mwizi, anakuja kukudai na fidia japo kakuibia!!! Usicheze na mikataba, jamaa wanawalipa pesa nyingi wanasheria na wanawapa muda mrefu kuset mikataba tata kuitatua pindi wakiburuzwa kortini. Je, ni pendekezo lipi la PAC alilosoma Zitto liliwagusa na kufanyiwa kazi? Je, wako wapi Meremeta Dip Green na hawa jamaa wa EPA? Si bado mikataba inawalinda na haki ya mwananchi inaendelea kutafunwa? Yaani uliyetajiwa ndie mwizi wako, bado unamlipa!!!

Wakati hayo hayajaisha, linakuja saga la Lugumi. Hili nalo tutapiga keleleee, then litaishia kama upepo wa jangwani. Ndio maana nchi kama Rwanda, China n.k wanakuwa na sheria kali, ukihisiwa tu una harufu ya wizi wanakuwahisha.....
 
Back
Top Bottom