Ogopa Taifa ambalo watu wake hawajaelimika

Ogopa Taifa ambalo watu wake hawajaelimika

Xperience

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2012
Posts
278
Reaction score
51
Kwa kawaida nchi zilizoendelea hazikuwa na matabaka makubwa sana katika karne ya 21 na tunaona mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi yanavyoshika kasi. Kwanza kwa chama chochote chenye kukaa madarakani kwa miaka mingi kama CCM na kuwatendea watu wake madhila makuu kama hivi sasa katika nchi nyingine ambazo watu wake wameelimika kisingekuwepo madarakani. Na kama watu hawajaeloimika hiyo tu ni sababu mojawapo ya uovu wa chama husika. Wanaoshabikia CCM ni wale ambao hawajui mbele wala nyuma juu ya demokrasia na maendeleo ya kiuchumi kwa ujumla. Kwa mfano mmoja aliniuliza chadema ikishika madaraka watagawa pesa. Nikamwambia watakachofanya ni kuondoa ugumu wa maisha ili pesa yako ndogo uliyo nayo inunue bidhaa kwa wingi huo ndo utatuzi wa ugumu wa maisha. Hilo wengi hawalijui. Na huo ndio mtaji wa vigogo wa CCM na watoto wao.Hivyo namalizia kwa kusema
 
ndo mana tunasema;
elimu
elimu
elimu.
 
Kama unahitaji mabadiliko ya kweli basi utayapata kwa Dr.JPM na si vinginevyo!
 
Siipendi CCM, japo namkubali MaPadlock na simkubali kabisa EL... sema kipindi hiki UKAWA wakipata nafasi naona itakua poa zaidi, after thinking nimeona jamaa yupo chini ya CCM hawezi kwenda against chama, lazima tu watamkaba.. EL akibanwa vizuri na UKAWA anaweza akafanya kitu, nahisi UKAWA wanaweza leta mabadiliko flani coz wamesota sana na hata wananchi nao wanawasukuma sana..

CCM wakirudi hata wakizembea wao washazoea wanachukua tu kila term, ndo maana hata bungeni walikua wanapuuza wapinzani sana. Inabidi sasa UKAWA wabebe kipindi hiki ili CCM wajifunze kua nchi hii ni ya wananchi sio ya chama.. wao ndo wageuke kua wapinzani
 
Mimi mwana CCM nimeamua kuipa CCM pumziko la milele.Kura yangu ni kwa LOWASSA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom