Ogopa matapeli

Ogopa matapeli

Nyati

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2009
Posts
2,528
Reaction score
1,917
Mapema mwaka jana nikiwa safarini kikazi kigoma nilikutana na kisa hiki:
Kuna daktari mstaafu anafundisha ktk chuo kimojawapo cha Afya mkoani hapo. Siku moja jumanne alipokea simu kutoka kwa mtu asiyemfahamu ambaye alijitambulisha kuwa alisoma na mwanae (akataja jina) hapo zamani, na alikuwa akiwatembelea nyumbani kwao wakiwa Dar Es Salaam.

Alimweleza kuwa anafanya kazi na shirika moja la kimataifa na wanatoa huduma za afya. Kwa wakati huo alikuwa amepata fedha za kufanya mradi wa kufundisha mafunzo kwa watumishi wa Afya ktk mikoa ya Kigoma na Tabora ktk awamu ya kwanza, kabla ya kuendelea ktk mikoa mingine. Alisema kuwa bajeti ni nzuri sana kwani wameomba wakitumia dola za marekani . Alimweleza kuwa anaomba msaada wa kutafutiwa wakufunzi na watoa huduma za chakula, kumbi za kufanyia mafunzo pamoja na mratibu “ Coordinator” wa mafunzo ya “Family planning”. Alimweleza kuwa wakufunzi watalipwa dola 150 kwa siku, mratibu dola 200 kwa siku, ukumbi wa kufanyia mafunzo ktk wilaya usizidi dola 500 kwa siku, pale mkoani usizidi dola 1000 kwa siku, huduma ya chakula na viburudisho vingine zisizidi dola 50 kwa kila mshiriki, na pia kila wilaya wataendesha workshop mbili za siku tano tano kila moja, na washiriki wasipungue 30 lakini wasizidi 35.

Yule mzee maskini alimweleza kuwa yeye ni mkufunzi wa masomo hayo na ana uzoefu wa muda mrefu. Basi yule kijana akamwambia kuwa kwa kuwa anamfahamu basi atamchukua yeye awe Mratibu na atalipwa dola 250 badala ya 200 kwa siku na pia kama anaweza ingia mkataba na watoa huduma za chakula na ukumbi wao watamlipa yeye kama ilivyoainishwa hapo juu. Mzee akanza “uratibu” kwa kutafuta wakufunzi wawili ambapo alipata walimu wenzie, na pia akatafuta huduma za chakula kwa bei ya chini kama shilingi elfu kumi hivi kwa kila mshiriki.

Siku ya jumatano yule kijana mwenye dili akapiga tena kuangalia kama amaefanikiwa na akajibiwa kuwa kila kitu kiko sawa. Mzee akaelezwa kuwa “mimi nipo uwanja wa ndege natoa vifaa vya mafunzo” ambavyo vingetumwa Kigoma kwa ndege kesho yake alhamisi. Mzee wa watu akajua mambo yanaiva kwani aliombwa “physical address” ili vifaa vipelekwe hapo moja kwa moja na kijana wao atakayevisindikiza!, mzee akafanya kama alivyoambiwa.

Alhamisi mchana akapigiwa simu kuwa mambo yameharibika kidogo kwani ATM imemeza VISA kadi yake hivyo ameambiwa na NBC kuwa ataipata ijumaa jioni kwani ATM azifunguliwa ovyo ovyo. Hivyo amekwama kupata pesa ya kulipia gharama za kusafirisha mizigo kwa Precision Air ambayo ndo ilikuwa na nafasi ya kuweza beba mzigo huo na kwa wiki husika hiyo ilikuwa safari ya mwisho. Hivyo itabidi waahirishe kuanza matayarisho ya mafunzo hadi wiki keshokutwa. Mzee wa watu akauliza ni shilingi ngapi, akajibiwa ni 960,000/= tu, basi mzee akamwambia watatoa pesa hiyo ili mambo yaende naye arudishiwe wakifika Kigoma, kijana akashukuru sana. Basi mzee wa watu pamoja na wale wakufunzi wakaingia mifukoni na kutuma kwa M-PESA. Kijana akashukuru sana na akasema mambo yataenda kama “walivyopanga”, na akasema wataipeleka mizigo hiyo Airport wakati huo ili ipelekwe kigoma kesho yake yaani ijumaa.

Baada ya masaa matatu hivi mzee akapiga kujua kama waliweza kuipeleka, simu ikawa haipokelewi, akajaribu tena ikawa hivyo hivyo akaendelea kujaribu kila mara wapi? Akampgigia mwanae ambaye yupo nje ya nchi kumuulizia juu ya rafiki yake huyo, kijana akasema hamjui mtu huyo! Mzee akaendelea kupiga na kwa bahati nzuri simu ikapokelewa lakini aliuzwa yeye ni nani badala ya shikamoo aliyokuwa amezoea. Akajitambulisah kuwa yeye ni “mratibu” wa mafunzo ya familia. Yule kijana akamwambia kuwa asiwasumbue tena, akamwambia kuwa tena tumekukadiria vibaya tungekuibia zaidi ya hizo, akaambiwa kuwa wewe kama ungekuwa na uwezo wa kupata dola 250 kwa siku usingekuwa unakaa huko porini. Mzee akamtisha kuwa asiporejesha pesa hizo atamgeuza nyau!, kijana akacheka akamjibu kuwa kama angekuwa na uwezo wa kuroga basi angeroga pesa ikahamia mifukoni mwake na asiwasumbue tena. Basi mzee wa watu akaandika maumivu. HIVYO TUWE MAKINI NA MATAPELI HAWA WANA MBINU MBALI MBALI.
 
hahahhaaa msomi mzima kapigwa kijinga sana.
 
Mapema mwaka jana nikiwa safarini kikazi kigoma nilikutana na kisa hiki:
Kuna daktari mstaafu anafundisha ktk chuo kimojawapo cha Afya mkoani hapo. Siku moja jumanne alipokea simu kutoka kwa mtu asiyemfahamu ambaye alijitambulisha kuwa alisoma na mwanae (akataja jina) hapo zamani, na alikuwa akiwatembelea nyumbani kwao wakiwa Dar Es Salaam.

Alimweleza kuwa anafanya kazi na shirika moja la kimataifa na wanatoa huduma za afya. Kwa wakati huo alikuwa amepata fedha za kufanya mradi wa kufundisha mafunzo kwa watumishi wa Afya ktk mikoa ya Kigoma na Tabora ktk awamu ya kwanza, kabla ya kuendelea ktk mikoa mingine. Alisema kuwa bajeti ni nzuri sana kwani wameomba wakitumia dola za marekani . Alimweleza kuwa anaomba msaada wa kutafutiwa wakufunzi na watoa huduma za chakula, kumbi za kufanyia mafunzo pamoja na mratibu " Coordinator" wa mafunzo ya "Family planning". Alimweleza kuwa wakufunzi watalipwa dola 150 kwa siku, mratibu dola 200 kwa siku, ukumbi wa kufanyia mafunzo ktk wilaya usizidi dola 500 kwa siku, pale mkoani usizidi dola 1000 kwa siku, huduma ya chakula na viburudisho vingine zisizidi dola 50 kwa kila mshiriki, na pia kila wilaya wataendesha workshop mbili za siku tano tano kila moja, na washiriki wasipungue 30 lakini wasizidi 35.

Yule mzee maskini alimweleza kuwa yeye ni mkufunzi wa masomo hayo na ana uzoefu wa muda mrefu. Basi yule kijana akamwambia kuwa kwa kuwa anamfahamu basi atamchukua yeye awe Mratibu na atalipwa dola 250 badala ya 200 kwa siku na pia kama anaweza ingia mkataba na watoa huduma za chakula na ukumbi wao watamlipa yeye kama ilivyoainishwa hapo juu. Mzee akanza "uratibu" kwa kutafuta wakufunzi wawili ambapo alipata walimu wenzie, na pia akatafuta huduma za chakula kwa bei ya chini kama shilingi elfu kumi hivi kwa kila mshiriki.

Siku ya jumatano yule kijana mwenye dili akapiga tena kuangalia kama amaefanikiwa na akajibiwa kuwa kila kitu kiko sawa. Mzee akaelezwa kuwa "mimi nipo uwanja wa ndege natoa vifaa vya mafunzo" ambavyo vingetumwa Kigoma kwa ndege kesho yake alhamisi. Mzee wa watu akajua mambo yanaiva kwani aliombwa "physical address" ili vifaa vipelekwe hapo moja kwa moja na kijana wao atakayevisindikiza!, mzee akafanya kama alivyoambiwa.

Alhamisi mchana akapigiwa simu kuwa mambo yameharibika kidogo kwani ATM imemeza VISA kadi yake hivyo ameambiwa na NBC kuwa ataipata ijumaa jioni kwani ATM azifunguliwa ovyo ovyo. Hivyo amekwama kupata pesa ya kulipia gharama za kusafirisha mizigo kwa Precision Air ambayo ndo ilikuwa na nafasi ya kuweza beba mzigo huo na kwa wiki husika hiyo ilikuwa safari ya mwisho. Hivyo itabidi waahirishe kuanza matayarisho ya mafunzo hadi wiki keshokutwa. Mzee wa watu akauliza ni shilingi ngapi, akajibiwa ni 960,000/= tu, basi mzee akamwambia watatoa pesa hiyo ili mambo yaende naye arudishiwe wakifika Kigoma, kijana akashukuru sana. Basi mzee wa watu pamoja na wale wakufunzi wakaingia mifukoni na kutuma kwa M-PESA. Kijana akashukuru sana na akasema mambo yataenda kama "walivyopanga", na akasema wataipeleka mizigo hiyo Airport wakati huo ili ipelekwe kigoma kesho yake yaani ijumaa.

Baada ya masaa matatu hivi mzee akapiga kujua kama waliweza kuipeleka, simu ikawa haipokelewi, akajaribu tena ikawa hivyo hivyo akaendelea kujaribu kila mara wapi? Akampgigia mwanae ambaye yupo nje ya nchi kumuulizia juu ya rafiki yake huyo, kijana akasema hamjui mtu huyo! Mzee akaendelea kupiga na kwa bahati nzuri simu ikapokelewa lakini aliuzwa yeye ni nani badala ya shikamoo aliyokuwa amezoea. Akajitambulisah kuwa yeye ni "mratibu" wa mafunzo ya familia. Yule kijana akamwambia kuwa asiwasumbue tena, akamwambia kuwa tena tumekukadiria vibaya tungekuibia zaidi ya hizo, akaambiwa kuwa wewe kama ungekuwa na uwezo wa kupata dola 250 kwa siku usingekuwa unakaa huko porini. Mzee akamtisha kuwa asiporejesha pesa hizo atamgeuza nyau!, kijana akacheka akamjibu kuwa kama angekuwa na uwezo wa kuroga basi angeroga pesa ikahamia mifukoni mwake na asiwasumbue tena. Basi mzee wa watu akaandika maumivu. HIVYO TUWE MAKINI NA MATAPELI HAWA WANA MBINU MBALI MBALI.

Inasikitisha sana ila tuwe makini zaidi.
 
hili ndo tatizo la kutaka vya bure, mzee namlaum sana kwanini hakushirikisha mwanae kabla?
 
Mapema mwaka jana nikiwa safarini kikazi kigoma nilikutana na kisa hiki:
Kuna daktari mstaafu anafundisha ktk chuo kimojawapo cha Afya mkoani hapo. Siku moja jumanne alipokea simu kutoka kwa mtu asiyemfahamu ambaye alijitambulisha kuwa alisoma na mwanae (akataja jina) hapo zamani, na alikuwa akiwatembelea nyumbani kwao wakiwa Dar Es Salaam.

Alimweleza kuwa anafanya kazi na shirika moja la kimataifa na wanatoa huduma za afya. Kwa wakati huo alikuwa amepata fedha za kufanya mradi wa kufundisha mafunzo kwa watumishi wa Afya ktk mikoa ya Kigoma na Tabora ktk awamu ya kwanza, kabla ya kuendelea ktk mikoa mingine. Alisema kuwa bajeti ni nzuri sana kwani wameomba wakitumia dola za marekani . Alimweleza kuwa anaomba msaada wa kutafutiwa wakufunzi na watoa huduma za chakula, kumbi za kufanyia mafunzo pamoja na mratibu “ Coordinator” wa mafunzo ya “Family planning”. Alimweleza kuwa wakufunzi watalipwa dola 150 kwa siku, mratibu dola 200 kwa siku, ukumbi wa kufanyia mafunzo ktk wilaya usizidi dola 500 kwa siku, pale mkoani usizidi dola 1000 kwa siku, huduma ya chakula na viburudisho vingine zisizidi dola 50 kwa kila mshiriki, na pia kila wilaya wataendesha workshop mbili za siku tano tano kila moja, na washiriki wasipungue 30 lakini wasizidi 35.

Yule mzee maskini alimweleza kuwa yeye ni mkufunzi wa masomo hayo na ana uzoefu wa muda mrefu. Basi yule kijana akamwambia kuwa kwa kuwa anamfahamu basi atamchukua yeye awe Mratibu na atalipwa dola 250 badala ya 200 kwa siku na pia kama anaweza ingia mkataba na watoa huduma za chakula na ukumbi wao watamlipa yeye kama ilivyoainishwa hapo juu. Mzee akanza “uratibu” kwa kutafuta wakufunzi wawili ambapo alipata walimu wenzie, na pia akatafuta huduma za chakula kwa bei ya chini kama shilingi elfu kumi hivi kwa kila mshiriki.

Siku ya jumatano yule kijana mwenye dili akapiga tena kuangalia kama amaefanikiwa na akajibiwa kuwa kila kitu kiko sawa. Mzee akaelezwa kuwa “mimi nipo uwanja wa ndege natoa vifaa vya mafunzo” ambavyo vingetumwa Kigoma kwa ndege kesho yake alhamisi. Mzee wa watu akajua mambo yanaiva kwani aliombwa “physical address” ili vifaa vipelekwe hapo moja kwa moja na kijana wao atakayevisindikiza!, mzee akafanya kama alivyoambiwa.

Alhamisi mchana akapigiwa simu kuwa mambo yameharibika kidogo kwani ATM imemeza VISA kadi yake hivyo ameambiwa na NBC kuwa ataipata ijumaa jioni kwani ATM azifunguliwa ovyo ovyo. Hivyo amekwama kupata pesa ya kulipia gharama za kusafirisha mizigo kwa Precision Air ambayo ndo ilikuwa na nafasi ya kuweza beba mzigo huo na kwa wiki husika hiyo ilikuwa safari ya mwisho. Hivyo itabidi waahirishe kuanza matayarisho ya mafunzo hadi wiki keshokutwa. Mzee wa watu akauliza ni shilingi ngapi, akajibiwa ni 960,000/= tu, basi mzee akamwambia watatoa pesa hiyo ili mambo yaende naye arudishiwe wakifika Kigoma, kijana akashukuru sana. Basi mzee wa watu pamoja na wale wakufunzi wakaingia mifukoni na kutuma kwa M-PESA. Kijana akashukuru sana na akasema mambo yataenda kama “walivyopanga”, na akasema wataipeleka mizigo hiyo Airport wakati huo ili ipelekwe kigoma kesho yake yaani ijumaa.

Baada ya masaa matatu hivi mzee akapiga kujua kama waliweza kuipeleka, simu ikawa haipokelewi, akajaribu tena ikawa hivyo hivyo akaendelea kujaribu kila mara wapi? Akampgigia mwanae ambaye yupo nje ya nchi kumuulizia juu ya rafiki yake huyo, kijana akasema hamjui mtu huyo! Mzee akaendelea kupiga na kwa bahati nzuri simu ikapokelewa lakini aliuzwa yeye ni nani badala ya shikamoo aliyokuwa amezoea. Akajitambulisah kuwa yeye ni “mratibu” wa mafunzo ya familia. Yule kijana akamwambia kuwa asiwasumbue tena, akamwambia kuwa tena tumekukadiria vibaya tungekuibia zaidi ya hizo, akaambiwa kuwa wewe kama ungekuwa na uwezo wa kupata dola 250 kwa siku usingekuwa unakaa huko porini. Mzee akamtisha kuwa asiporejesha pesa hizo atamgeuza nyau!, kijana akacheka akamjibu kuwa kama angekuwa na uwezo wa kuroga basi angeroga pesa ikahamia mifukoni mwake na asiwasumbue tena. Basi mzee wa watu akaandika maumivu. HIVYO TUWE MAKINI NA MATAPELI HAWA WANA MBINU MBALI MBALI.

So sad,, Ila mtego huo ni mkali hata msomi gani angenasa.
 
Asante Mkuu, taarifa hii tuiwekee umakini... wengi tumesha tapeliwa kinamna.
 
Mzee alijua kaokota dodo katika mkorosho,yaani kirahisi tu mtu akuletee dili kubwa kama hilo miguuni kwako?......
 
hili ndo tatizo la kutaka vya bure, mzee namlaum sana kwanini hakushirikisha mwanae kabla?

na mimi nashangaa kwanini hakumuuliza mwanae kabla???

Mwanae anakaa nje ya nchi na majira ni tofauti kidogo nafikiri ndo maana aliacha kumpigia. lkn pia pale mwanzoni hakukuwa na ishara zozote za hatari
 
Hata mimi nilipigiwa na wataalamu wa madawa ya mifugo kutoka Manyara nikachukue Mikocheni kwa Sh 950,000/= kisha nipeleke sampo Seaclif kwa wazungu na tenda ikitiki tungepata kama mil. 6 Nilistuka lakini nilishaanza safari yakuelekea benki mlimani city kuchukua pesa nilirudia ubungo baada ya kumshinda shetani wa tamaa. Baadaye nikawa nawapigia "wazungu kuwaenjoy" kutokana na kujiona mjanja. Kutapeliwa kunatokana na tamaa ya kupata pesa za haraka haraka. Wengine walinitumia msg kuwa nimeibuka mshindi wa sh. miliomni 10 katika promotion ambayo sijawahi kushiriki hivyo nitume pesa ili nipewe pesa. Matapeli wako smart wanawatapeli hata makamanda wa polisi wa mikoa na mawaziri na wengine mpaka serikali nzima wanaitapeli. Si mnakumbuka issue ya Richmond. Baraza zima la mawaziri pamoja na mwenyekiti wao walitapeliwa sasa tunalipa fidia watanganyika wote! Imekula kwetu!
 
hili ndo tatizo la kutaka vya bure, mzee namlaum sana kwanini hakushirikisha mwanae kabla?

Usimlaumu. Ujinga hauna mwenyewe. We hukumbuki serikali yote ilivyotapeliwa na Richmond. Fikiria baraza lote la mawaziri mpaka mwenyekiti kuna maprofesa, madaktari na wachumi mule lakini walitapeliwa. Huyo mzee ni cha mtoto! Muonee huruma.
 
Back
Top Bottom