Mtoto Wabibi
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 451
- 294
Jimbo la Isimani-Iringa limekuwa na changamoto nyingi huku mbunge wa jimbo hilo mh.willium lukuvi (CCM) akiwa amekalia kiti hicho tangu 1995 hadi leo hii na akiwa ameshika nyazifa kubwa kubwa serikani tangu kipindi hicho lakini bado ameendelea kuwaotesha ndoto wanaisimani.
Nashindwa kuelewa kwanini huyu mh. Lukuvi anasifiwa sana kitaifa wakati jimboni kwake ni shida na changamoto zilizokomaa tangu uhuru hadi leo hakuna chochote.leo naanza na ofisi yake kabisa ya jimbo la Isimani.
Huku serikali ikiendelea kujadili kuhusu uhamishaji wa ofisi za serikali Dodoma cha kushangaza ofisi ya jimbo la mbunge huyu haipo jimboni kwake hadi leo hii.ofisi ameweka Iringa mjini ambalo ni jimbo la Mchungaji msingwa wa CHADEMA ( kwa kifupi ipo chini ya Msigwa kwa sababu ipo katika eneo la Msigwa) na isitoshe yeye ni wa Dar es Salaam kwa hivi sasa hata Iringa yenyewe anaikimbia japo ndio maskani yake huko tarafani Idodi. yani ni sawa na nchi ya Tanzania lakin makao makuu yake yawe Newyork na sio hapa Tanzania eti kwa kuwa marekani kuzuri na kuna miundombinu mizuri.
Swali langu ni:
1: kwanini kwa kipindi hiki chote Ofisi za jimbo hazijajengwa jimboni Isimani?
2: Hata kama miundombinu mibovu au huduma za kijamii ni mbovu, je hujaona sababu ya kuboresha kwa kipindi hicho chote kujenga na kuweka ofisi jimboni kwako?
3: Utawasumbua hadi lini wananchi wako kufuata ofisi yako huko jimboni kwa Msigwa Iringa mjini
4: Ghalama za kufuata ofisi yako huoni kama unawaongezea umasikini wananchi wako?
5: Muda wanaopoteza pia huko ugenini unaujua?
Unakuta mtu anaenda ugenini hana ndugu wala rafiki isitoshe pale ofisini kwako wanaangalia sura kwanza ndio uhudumiwe sijui ndio unavowaagiza au lah.
wananchi wanateseka sana. wanataka na sio kuomba tena OFISI IHAMIE ISIMANI JIMBONI na sio jimboni kwa Msigwa.
By mtoto wa bibi