Ofisi ya Rais iajiri mwandishi wa Hotuba za Rais Magufuli

Iceman 3D

JF-Expert Member
Sep 3, 2016
20,611
67,091
Jana nimesoma kitabu cha "uwazi na ukweli" chenye hotuba mbali mbali za Rais Mkapa miaka ya 2000. Sasa nikawa sipati picha mwaka 2040 pale mwanangu atakapo kuja kupata kitabu cha rekod za hotuba za Magufuli, ata jifunza kitu gani!? na atafikiri Magufuli alikuwa Rais wa namna gani kwa maneno yake haya!?

Nimefuatilia kidogo namna Rais Magufuli anavo hutubia, mara nyingi inakatisha tamaa ukimsikiliza, pengine yeye huwa anaona watu wana cheka ila nadhani wengi huwa wana mcheka yeye na hawacheki anacho kiongelea.

Ukijikumbusha maneno aliyo yazungumza Zanzibar, Singida na kagera na alipokuwa ana zungumza kanisani bukoba, inashangaza kuona rais anaongea maneno ya ajabu na yanayo katisha tamaa wananchi wake. Saa nyingine yanatishia usalama na amani ya nchi. Hata siku alipo kuwa ana mkaribisha Rais wa Zambia ilikuwa ni moja ya hotuba mbaya za ki diplomasia nilizowahi kuziona.

Tatizo ni kuwa nahisi huyu bwana hana mwandishi wa hotuba, na kama yupo basi hafanyi kazi yake. najua kuna wachache wanao sema Rais huwa hazunguki ana ongea ukweli, lakini mara nyingi Rais akizungumza maneno yake yana kosa ustaarabu, ubinadamu, staha na usomi, yote hii ni kwa sababu rais ana ropoka tu na hakai kutafuta lugha ya kusemea ukweli ikiambatana na kuwa mstaarabu au kuwa na ubinadamu.

Hotuba iliyo andikwa itamsaidia atamke vitu kwa lugha fasaha, na kwa mpangilio mzuri na wenye sababu kwa kila anacho zungumza, pia haita ondoa idea ya uhalisia wa fikra zake ila utaziweka fikra zake kwenye mpangilio mzuri, kwa kuwa mwandishi hata andika kitu chake ila ataandika fikra za Rais.

Kwa kuwa rais wetu anaonekana kabisa hana washauri na huwa hasikilizi ushauri, uandishi wa hotuba utamfanya at least kujikosoa mwenyewe katika mpangilio wa mawazo yake, pia itakuwa hata kama akitaka aipambe idea yake zaid nje ya maandishi ya kwenye hotuba, bado akirudi kwenye hotuba ita fafanua zaidi.

Hata tatizo la lugha alilo nalo hasa ki inglish, halitakuwa na shida kama kuna mwandishi wa hotoba halafu na yeye akaisoma, japo hata kiswahili kinaonekana kumsumbua sana, bado uandishi wa hotuba utamsaidia kukinyoosha kiswahili chake, ila akipiga free style lazima iwe majanga.

Wapo baadhi ya watu huwa wanajiuliza, ilikuwaje mtu kama huyu akapata PhD? Jibu ni simple ni kwakuwa mawazo yake aliyaandika kwanza, akampa mtu ayapitie ndio akaenda ku present, na hata akitaka awe na hotuba zenye maana basi awepo mtu anaye mwandikia hotuba zake zipitiwe vizuri na ndiposa azungumze na wananchi.

*Rais Magufili dunia yako, chaguo lako, chagua kumuweka mwandishi wa hotuba zako tafadhali.
 
Kila MTU anamfumo wake sio wote watafanana mbona nyerere hotuba zake nyingi alikuwa haandikiwi? Na Mbona mnazisikiliza mpaka leo. Tatizo watanzania tumezoea kukariri vitu
 
Kingereza gani hicho, kiswahili gani hicho ni mzaliwa wa mkoa wa mara (musoma) hicho kiswahili cha jamaa nashindwa kukielewa hata IDD AMIN aliongea kiswahili kizuri hata okello wa mapinduzi zenji pia
 
Back
Top Bottom