Simon Templar
Member
- Mar 3, 2016
- 18
- 21
Kuna taarifa kwamba, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) imetuhumiwa kupokea Shs. 30 milioni ili kuzima kesi ya mauaji ya mwanafunzi Joel Chacha kabla haijafikishwa mahakamani.
Machi 21, 2016 baba wa marehemu, Peter Chacha, amemwandikia barua Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji George Masaju akilalamika kuhusu kesi hiyo yenye kumbukumbu ya polisi namba OB/IR/8304/2014 akilalamika kwamba kuna hujuma zinazotaka kufanywa na ofisi ya DPP kuizima kesi hiyo.
Barua hiyo inaeleza kwamba, ingawa tayari mtuhumiwa wa mauaji hayo, Andrew Sanga, yuko mahabusu baada ya kukamatwa Februari mwaka huu, kumekuwepo na taarifa kwamba ndugu wa mlalamikaji wamekuwa katika harakati za kukusanya fedha ili kuizima kesi hiyo.
"Mimi nilipata taarifa kutoka kwa msiri wangu aliyeko mkoani Mbeya kwamba kuna fedha kiasi cha Shs. 30 milioni zimechangwa na wazazi wa mtuhumiwa Andrew Sanga na zimepelekwa kwa mwanasheria wa serikali anayeshughulikia kesi hiyo," anasema Chacha katika barua yake kwenda kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Chacha anasema kwamba, baada ya taarifa hizo aliamua kuja Dar es Salaam kutoka Mbeya ili kumuona DPP Biswalo Mganga kwa nia ya kujua mwenendo wa kesi pamoja na kumpatia taarifa hizo, lakini kwa mshangao wake, anasema Machi 21 alipokutana naye DPP alimwambia kwamba mtuhumiwa hana hatia na ameagiza aachiliwe.
"(DPP) alinijibu kwamba kesi hiyo amekwisha itolea uamuzi ya kwamba mtuhumiwa hana hatia hivyo ameelekeza aachiliwe huru," anasema Chacha kwenye barua hiyo.
Habari za kipolisi zinaeleza kwamba, marehemu Joel, ambaye wakati mauti yanamkuta alikuwa na miaka 18, alikuwa mwanafunzi wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari Feza Boys iliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam, ambapo alikutwa amekufa katika mazingira ya kutatanisha wakati akiwa anaogelea katika ufukwe wa Coco Beach pamoja na mtuhumiwa.
Tukio hilo, kwa mujibu wa taarifa za kipolisi, lilitokea Jumapili, Septemba 7, 2014 majira ya saa 10 jioni na baada ya tukio hilo mtuhumiwa, ambaye aliondokea kuwa rafiki wa ghafla wa marehemu wakati akiwa likizo nyumbani kwao Mbeya, hakuwahi kutoa taarifa kwa wazazi wa marehemu wala shuleni kwake japokuwa maiti ilikuwa imechukuliwa na polisi siku hiyo na kwenda kuhifadhiwa kwenye Hospitali ya Mwanyamala.
Mbali ya hivyo, mtuhumiwa, ambaye simu yake ndiyo iliyotumiwa na marehemu kuwasiliana na ndugu zake mara ya mwisho saa 8:30 mchana kabla mauti hayajamkuta, alitoweka nchini Septemba 11, 2014 (siku nne baadaye) na haikujulikana mahali alikokwenda hadi mwaka 2015 wakati ilipobainika kwamba alikimbilia India kwa madai kwamba alikuwa anasoma.
Hata hivyo, taarifa ya daktari aliyeufanyia uchunguzi (post mortem) mwili wa marehemu ilieleza kwamba, kifo chake kilisababishwa na kuvunjwa shingo na siyo kuzama majini kama ilivyokuwa imeelezwa awali.
Nitarudi baadaye kuelezea undani wa tukio hili.