Nyumba zaidi ya 150 za teketea kwa moto Afrika Kusini

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,245
2,000
Watu takriban 10,000 wamelazimika kukimbia makwao kutoka mji mmoja pwani ya Afrika Kusini ambao umeharibiwa pakubwa na moto.


Wanajeshi wanashiriki katika juhudi za kukabiliana na mtaa huo kukabili moto huo ambao unawaka katika maeneo 25 katika mji wa Knysna.

Watu wanane wamefariki kutokana na upepo mkubwa na moto ambao umekumba mji huo na maeneo mengine katika kanda ya Cape Magharibi.


Upepo huo mkubwa umesaidia kueneza moto huo.

Nyumba zaidi ya 150 zimeteketezwa eneo hilo kwa mujibu wa shirika la wazimamoto.
Mji huo una takriban wakazi 77,000.

Unapatikana kilomita 500 mashariki mwa mji wa Cape Town.

Jeshi la Taifa la Afrika Kusini litasaidia kuangusha mabomu ya maji yanayotumiwa kuzima moto kusaidia kukabili moto huo, msemaji wa jeshi Simphiwe Dlamini amesema.

Wanajeshi karibu 150 watatumwa eneo hilo kuzuia wahalifu kupora mali katika maeneo ambayo wenyewe wamekimbia.

Mwezi Mei, mkoa wa Cape Magharibi ulitangaza janga ya ukame baada ya mabwawa mawili makubwa kukauka kabisa.

Chanzo: BBC
 

mwasu

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
10,208
2,000
Juzi ilikuwa kimbunga nyumba zikaharibika leo moto tena, Mungu wape faraja wahanga hawa, inasikitisha sana.
 

shatisuruali

JF-Expert Member
Jul 28, 2016
604
1,000
Ni slums?? May be serikali inataka kuporomosha madude. Maana siyo kwa nyumba zote hizo. Zingekuwa zimepangiliwa zisingewaka ivo. POLE ZAO
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom