Mdau ni bora uende ukaone msingi wa hizo nyumba maana wako kwenye foundation sasa. Zipo hapo ilala boma, kama unatokea kigogo ni kuna barabara kushoto inayotizamana na jengo la Mkuu wa koa kulia kwake. Zinaonekana tu barabarani bati la uzio. Ukweli sq metres za nyumba 115.8 ni ndogo sana hata vymba vyake, longe, dining, jiko na facility nyingine ni kwa ajii ya nucleous family tu. Ukweli nyumba zile wataishia kununua wahindi, wapemba, waarabu, wasomali na watu kama akina maige na ngeleja na mafisadi wengine. Kwa mtanzania wa kawaida anayetafuta pesa kwa taabu ni ngumu sana kulipa millioni 200 kwa nyumba kama ile. Hata kama iko karibu na mjini but si kivile sana maana mitaa yenyewe iko kama uswahilini tu. Halafu kitu kingine, zile nyumba naona sewage tanks zitakuwa hapo, maana kwenye ramani kubwa ndivyo inavyoonyesha, ambapo itakuwa ni tabu sana kwa fmilia 48 plus wakazi (multiply by 6) kwa nucleous famili ndo utapata idadi kamili (mama, baba, watoto 4) hapo maid/houseboy bado maana hakuna quarters zao. Vinginevyo waseme kama wataunganisha katika sewer system.
Ninatoa ushauri kwa NHC kama wanatembelea humu kuwa:
1. Wajaribu kujenga nyumba zenye hadhi, kwa standard sizes, hakuna mtu analala tena chumba cha sq metre 10, ilishapitwa na wakati. Vyumba vya kawaida ventilated na ukitegemea polution ya DSM ni bora viwe Sq 12-16 na cha master kiwe 20-36, Dining na jiko pia viwe spacious.
2. Jengeni nyumba pia kwa kupanga vizuri aina ya wateja. Kwa mteja wa nyumba ya bei kubwa ni lazima awe ni mtu ambaye ana maisha fulani mazuri hivyo ni mtu wa quality, kwa mantiki hiyo nyumba za jirani na mjingi ziwe na quality stahiki kama ukubwa wa kutosha, ventilated, not in squarters, etc.
3. Jaribuni kuangalia bei za nyumba zenu, hasa pale ambapo mnunuzi ni Mtanzania ongeeni na Serikali ili waondoe VAT kwa watanzania, hii itasaidia kupunguza bei kidogo kama kweli lengo ni kuwezesha watanzania wa kawaida na si wahindi na mafisadi.
4. Muda wa kulipa nyumba ndani ya miezi mitatu, mtanzania wa kawaida anawezaje hizo mili 200? Labda awe mwizi!!! Muda kwa kulipa hasa inapotekea ni mfanyakazi wa serikali uongezwe hadi miaka mitano.
5. ni kweli NHC mmekuwa na mortigage partners, but nasema si partners bali are supper business people. Huwezi kuwa na 18% for 15 years eti ni riba, riba ya mkopo wa mortigage ni vema iwe single digit and at most 10%. Imagine unataka mkopo say 60 mil for ten years utalipa faida like 70 mil plus principle ambayo 130 for 10 years. Hapo bado 3% up front processing fees, bado life and property insurances ambazo unalipa annualy jumla zote kama 1%. Sasa ni mtanzania yupi anawezeshwa hapa? Hata kama NHC wanajiendesha kibiashara but jua kuwa viwanja hivyo vilikuwa ni mali ya serikali ikiwa chini ya shirika la nyumba miaka hiyo.
Nampongeza sana DG Nehemiah Mchechu but try to look and behave like your fellow Tanzanians!!! Siyo wote ni matajiri na wanapata mshahara mkubwa kama wewe. Wewe na team yako nzuri try to be considerate, tunapenda nasi tupate nyumba potential areas na jirani na mjini ili tuwahi kazini but we cannot afford!!!!