Wakuu habari na poleni na majukumu. Kwa heshima na taadhima naomba mwenye kujua utaratibu utakaoniwezesha kupata nyumba ya kupanga ya nhc ndani ya Dar es salaam kwa gharama ya kitanzania, nyumba yenye vyumba viwili na sebule. Nashukuru sana. Kwa msaada tuwasiliane pm.
Inabidi utembelee ofisi zao Mkuu, Wana ofisi tofauti kulingana na eneo unalotaka kupanga, kuna form za kujaza alafu ikipatikana nyumba utatafutwa! Ukijaza form utakua kwenye list ya wanaosubiri