#Dubu,
Eti.... "Watu wasije wakapanga milele wakijua nyumba zote bei gani?" dadavua zaidi sijakuelewa...
Kuna tabia ya watanzania kuona kwamba kila mmoja kujenga ni ufahari! Binafisi siamini hivyo, na ndiyo maana makazi yetu ni full kizungumkuti, afya zetu zinazungukwa na mazingira hatarishi ya hali ya hewa kisa kila mmoja kutafuta kuishi mkwake!
Binafsi najua ujenzi si kazi rahisi lakini kadili watu wanavyo tafuta makazi yao ni kama ujenzi ni rahisi sana. Ila bado watu wengi waelewe kuwa kati ya sifa za nyumba bora si tu nyumba kuwa na choo, jiko na bafu pekee! Ni zaidi ya hapo, lazima nyumba bora iwe na yafutayo japo kwa uchache
1. Kiwanja kilichopimwa
2. Huduma muhimu ziwepo mfano barabara, maji, umeme, shule, hospitali
3. Mazingira mazuri yanayo zunguka nyumba, hii ni pamoja na hali nzuri ya hewa na mzunguko safi wa hewa
4. Mfumo wa maji taka, uratibu mzuri wa utupaji na ukusanyaji taka
etec,
Hakika NEMC wana kazi kweli kweli....!