Nyumba mpya inauzwa bei ya kutupwa

Nyumba mpya inauzwa bei ya kutupwa

mseseve weka bei. Then je Ina hati? unaweza weka mchoro wa ramani yake na iko umbali gani toka morogoro road?

Nimeongea nae haina hati kwa bei ongea naye wewe mwenyewe kwa kuwa ni suala binafsi katika kupatana. Mimi nimeona ni ghali kidogo, ngoja nisikilizie maana nimeona huruma sana sema sasa sina hela za kiasi kile. Pole mama yetu.
 
Nimeongea na mama na bei amenitajia, ila nionavyo mimi kwa bei ile na mahali ilipo nyumba Majohe ni ghali kwa kuwa pia finishing kubwa bado. Mshaurini mama aanzie bei ambayo si kubwa sana. Kwa bei aliyonitajia itamchukua muda mrefu kupata mteja.

Kakutajia bei gani? Mi kanitajia bei ndogo 30m.
 
Loh, najaribu kupata picha angekuwa mama yangu!! Dah, hana hata watoto wakubwa? Tujiwekeeni misingi endelevu jamani kabla umri haujatutupa mkono.
 
Heeee mbona mimi kanitajia mara tatu yake ila kasema inaongeleka?? Kwa ukubwa wa nyumba na kuwa finishing kubwa bado kabisa maana hata umeme haina ila anatumia solar. Hakika hata yeye amesema bado kabisa kumalizia kwa hiyo kwa mnaofahamu finishing ya nyumba basi utajuwa kuwa kuna mwendo mrefu.
 
Na utamu wa nyumba ni ktk finishing,hapo ni lazima ufunge mkanda,ila kwa mtu anayetaka kumsaidia mama basi na afanye hivyo,maana upo uwezekano hata ugonjwa wake umesababishwa na presha za kazi ya ualimu.
Mungu huyu angewapa ufunuo hawa wabunge wetu na kuzikataa posho ili ziweze kuwasaidia walimu wetu.
 
Loh, najaribu kupata picha angekuwa mama yangu!! Dah, hana hata watoto wakubwa? Tujiwekeeni misingi endelevu jamani kabla umri haujatutupa mkono.

nimeongea nae nikajikuta machozi yananitoka, nimemkumbuka Mama yangu Kule kijijini....najuta kumpigia. Sikujiskia amani kabisa nadhani Yuko kitandani. Tuwatunzeni wazazi wetu hata kama walitufanyia mambo madogo au hawakufanya kabisa
 
Very sad mpwa wangu, na watu watainunua tu hiyo nyumba tena kwa bei ya mkaa, kuna watu wana roho ngumu! Loh!
 
Bei gani mmetajiwa?
Mnamuonea huruma wakati mnaogopa kumfanyia promo?
 
Heeee mbona mimi kanitajia mara tatu yake ila kasema inaongeleka?? Kwa ukubwa wa nyumba na kuwa finishing kubwa bado kabisa maana hata umeme haina ila anatumia solar. Hakika hata yeye amesema bado kabisa kumalizia kwa hiyo kwa mnaofahamu finishing ya nyumba basi utajuwa kuwa kuna mwendo mrefu.

Finishing acha kabisa, ni uwendawazimu na lazima ugombane na mafundi kama ujenzi wako ni wa kimaskini wa kutafuta fundi mwenyewe kwa kila eneo la finishing. Kwakifupi finishing ni kati ya 30-40 hadi ikamilike kila kitu kwa kiwango cha wastani kwa nyumba kama ile. Ila kwa mwenye kuihitaji anaweza kulipa kati ya 35-45 si mbaya kumsaidia bi mkubwa wetu jamani
 
Nimeongea na mama na bei amenitajia, ila nionavyo mimi kwa bei ile na mahali ilipo nyumba Majohe ni ghali kwa kuwa pia finishing kubwa bado. Mshaurini mama aanzie bei ambayo si kubwa sana. Kwa bei aliyonitajia itamchukua muda mrefu kupata mteja.

Hebu tudokeze, amekutajia ngapi.

Tiba
 
ushauri wako waitajika pia kwa unavyoona wewe ungemwambia na kumshauri ni bei gani inayofaa
 
Promo inahitajika kwa ajili ya kununua coz hakuna msaada mwingine zaidi ya kuinunua nyumba ile na mwenyewe kesha sema anataka kurudi kijijini kwake akakae na ndugu zake wa karibu ili waweze kumhudumia na pia kama atapata seheemu anaweza akaendeleza taaluma yake kwa kufungua sehemu ya kufundishia kama tuition center hukohuko kijijini.mjini kila kitu ni hela na kama ukimpa msaada wa hela maana kila siku awe anasaidiwa tuu? leo mtamsaidia kesho mtachoka atarudi hali ileile...
 
Ni kweli usemavyo mkuu, kwa hiyo kumbe bado anayo energy ya kufanya kazi. Je alikuwa mwalimu wa ngazi gani? Kwao kabisa ni wapi? Anaweza kuuza hiyo nyumba, kisha akaenda kununua nyumba mkoani/wilayani kwake, akasajili shule ya awali na kutumia hiyo nyumba kama day care na kindergarten, akipata na mwalimu mwenzake mmoja wanaunganisha nguvu wanaweka sehemu ya kuwaingizia kipato kizuri tu, otherwise akakimbizane na kazi za shamba na ufugaji ambao unahitaji mtu active sana. Kila la heri mkuu, wana jf tunamuincourage apambane na changamoto iliyo mbele yake, msalimie sana bi mkubwa mwambie namwamkia, heshima kwake!
 
Finishing acha kabisa, ni uwendawazimu na lazima ugombane na mafundi kama ujenzi wako ni wa kimaskini wa kutafuta fundi mwenyewe kwa kila eneo la finishing. Kwakifupi finishing ni kati ya 30-40 hadi ikamilike kila kitu kwa kiwango cha wastani kwa nyumba kama ile. Ila kwa mwenye kuihitaji anaweza kulipa kati ya 35-45 si mbaya kumsaidia bi mkubwa wetu jamani

Kweli mkuu, hata mimi angeanzia hata 40 ili maongezi yaanzie pale. Mahali ilipo nyumba ni changamoto. Ungeisogeza maeneo mengine bei ingekuwa kubwa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom